Katumbi wa TP Mazembe arejea DRC

"Moise Katumbi ni kiongozi wa pekee wa upinzani nchini Congo ambaye ana ushawishi mkubwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa raia wa Congo".

Katumbi wa TP Mazembe arejea DRC

"Moise Katumbi ni kiongozi wa pekee wa upinzani nchini Congo ambaye ana ushawishi mkubwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa raia wa Congo".

20 May 2019 Monday 00:00
Katumbi wa TP Mazembe arejea DRC

MMILIKI wa klabu ya TP Mazembe ya DRC, Moise Katumbi leo Mei 20, 2019 amerejea nchini humo na kulakiwa na  maelfu ya wafuasi mjini Lubumbashi baaya ya kuishi uhamishoni kwa takribani miaka mitatu.

Katumbi ambaye pia ni kiongozi wa upinzani nchini humo amepokewa na maelfu ya wafuasi waliojawa na furaha na shangwe katika uwanja wa ndege wa Luano nchini Congo.

Kiongozi huyo amekuwa akiishi uhamishoni kwa miaka zaidi ya miwili iliyopita baada ya kushtakiwa na serikali ya rais wa zamani Joseph Kabila kwa makosa kadhaa ya uhalifu ukiwemo udanganyifu, kuwajiri maamluki na kujipatia uraia wa pili kinyume cha sheria.

Umati ulionekana ukimsindikiza Moise Katumbi kuelekea katika uwanja wa michezo wa TP Mazembe.

Katika mahojiano na televisheni, Katumbi alisema  anapanga kurudi nyumbani Mei 20 - ikiwa ni takriban miaka mitatu tangu aondoke nchini.

"Ni hakika kwamba Mei 20, 2019 nitakuwa Lubumbashi," Katumbi amenukuliwa na katika mahojiano hayo yaliofanyika Mei 6,2019.

Alieleza kwamba baada ya kurudi Lubumbashi anapanga ziara ya kitaifa katika alichotaja kuwa ni 'kuwaliwaza' raia wa DR Congo, hususan "familia zilizoteswa  na walioishi katika tabu".

Mnamo 2016, Moise Katumbi, alihukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kwa kununua nyumba kinyume cha sheria kwenye mji ulio mashariki mwa nchi wa Lubumbashi na pia kutuhumiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni ili kupanga njama dhidi ya serikali.


Wakati wa kuapishwa kwake, Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tshisekedi, aliahidi kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa wakiwemo watu wote waliofungwa wakati wa maandamano yaliyofanyika kabla ya uchaguzi wa mkuu wa mwezi wa Disemba mwaka jana.

Mashtaka dhidi ya Katumbi mwanasiasa mwenye umri wa miaka 54 yametupiliwa mbali chini ya utawala wake Tshisekedi, na kutoa fursa leo kwa Katumbi kurudi nyumbani.

Hatahivyo mpinzani huyo ameeleza kwamba uamuzi wa mahakama kubatilisha hukmu ya miaka mitatu dhidi yake sio kutokana na makubaliano na rais Félix Tshisekedi, badala yake mfumo wa sheria ambao sasa hauingiliwi kisiasa.


Katumbi, na Jean Pierre Bemba, kigogo mwingine wa upinzani Congo walimuunga mkono Martin Fayulu, katika uchaguzi mkuu nchini humo ambao Tshisekedi alichaguliwa rais.


Katumbi ni kiongozi wa upinzani ambaye amekuwa uhamishoni kutoka DR Congo baada ya kutengana na Rais Joseph Kabila.


Katumbi, alijiunga na upinzani mnamo 2015 baada ya kukosana na rais Joseph Kabila, wakati huo.

Katumbi ambaye amewahi kuwa Gavana wa jimbo tajiri zaidi nchini humo, Katanga alijiuzulu na kumshtumu rais Kabila kwa uongozi duni.

Moise Katumbi ni kiongozi wa pekee wa upinzani nchini Congo ambaye ana ushawishi mkubwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa raia wa Congo.

Alitangaza kutaka kuwania urais mwaka 2016, kabla ya uchaguzi huo kuahirishwa. Na mwaka jana alizuiwa kuingia nchini kugombea urais katika uchaguzi wa Desemba, aliyoushinda Tshisekedi.


 

Updated: 21.05.2019 09:30
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.