Kauli ya Magufuli yamleta Kaheza simba

Kauli ya Magufuli yamleta Kaheza simba

25 May 2018 Friday 09:45
Kauli ya Magufuli yamleta Kaheza simba

Na Amini Nyaungo

Klabu ya Simba imeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli juu ya kutengeneza kikosi kitakachokuwa imara kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Klabu hiyo imemshusha nyota wa Majimaji Marcel Boniventure Kaheza ambaye amefanya vizuri msimu huu kwa kupachika magoli 13 ya ligi kuu Tanzania bara.

Mchezaji huyo ambaye amewahi kuwa sehemu ya kikosi cha pili cha Simba miaka ya nyuma sasa anarudisha majeshi katika kikosi hicho ili kuwaongezea nguvu kwa washambuliaji waliopo kikosini hapo John Bocci na Emanuel Okwi.

Inasemekana bosi wa timu hiyo Mohamed Dewji alimtumia tiketi ya ndege ili kumalizana na chama la Msimbazi.

Rais Magufuli aliwaambia wazi kuwa kwa aina ya mpira wanaoucheza Simba haoni kama timu hiyo itaenda kufanya vizuri kimataifa, ambapo Simba watawakilisha nchi katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika msimu ujao baada ya kutwa kombe la ligi kuu Tanzania bara.

Azania Post

Updated: 25.05.2018 15:12
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
majasho king 2018-05-25 21:25:27

inaonekana Simba wanajinga vilivyo kwaajili ya msimu ujao tujipen hongera wana msimbaz

Avatar
Deogratus Emanuely 2018-06-18 23:46:53

Kwanza kabisa, naipa hongera timu yangu kwa uongozi mzuri na usajili pia, lakin kwanin niyonzima mmemtema maana najua yeye alikuwa bado hajapata nafas vizur mngempa nafasi ya kucheza msim wa mwisho ushaur lakn mim ni shabik mzur wa msimbaz mjuwe? afu na angalien washambuliaj ving'ang'aniz na wasumbufu mbele mjuwe mwakan kimataifa eti.