Kauli ya Rais wa chama cha soka Hispania hii hapa

Kauli ya Rais wa chama cha soka Hispania hii hapa

13 June 2018 Wednesday 16:15
Kauli ya Rais wa chama cha soka Hispania hii hapa

Rais wa Shirikisho la Spain - Luis Rubiales anaeleza chanzo za kumfukuza Lopetegui, baada ya kusaini mkataba na Real Madrid wakati nchi yake ikiwa ndiyo kwanza inaanza kushiriki katika kombe la dunia.

Kocha huyo inaonesha hakuwa na subira, angesubiri michuano kuisha ndiyo aweze kuongea na timu nyingine.

“Tumelazimika kusitisha mkataba wetu na Lopetegui kwa sababu ya tabia yake aliyoionyesha. Amekuwa kocha mzuri kwetu lakini hatuwezi kukubaliana na kitendo alichofanya. Makubaliano yake Madrid yamefanyika bila sisi kufahamishwa, tulikuja kufahamu kuhusiana na hili dakika 5 kabla ya Madrid kutangaza," amesema.

Rais huyo amesema kuwa amezungunza na wachezaji na wamemuhakikishia watafanya vizuri.

“Nimezungumza na wachezaji kabla ya kutangaza uamuzi huu na wamenihakikishia kwamba watakuwa na michuano mizuri,"

“Ni kweli baadhi ya wachezaji wakiongozwa na nahodha walinifuata mimi na viongozi wenzangu kujaribu kuzuia uamuzi huu lakini baada ya kufikiria kwa kina, tumefikia maamuzi haya,” amesema.

Kocha mpya atatangazwa muda wowote kuanzia leo ambapo michuano hiyo itaanza kesho.

Azania Post

Keywords:
Luis Rubiales
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.