Kelvin John atoa la moyoni kuhusu Taifa Stars

Kelvin John atoa la moyoni kuhusu Taifa Stars

20 June 2019 Thursday 09:48
Kelvin John atoa la moyoni kuhusu Taifa Stars

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

NYOTA wa timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Kelvin John ‘Mbappe’ amesema amejifunza mengi katika  kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na fainali za mataifa ya Afrika nchini Misri.

Kelvin  ambaye aliitwa kwenye kikosi hicho kwa lengo la kupata uzoefu mapema kutokana na kufanya kwake vizuri akiwa na Serengeti Boys, alisema amejifunza nidhamu  kutoka kwa kaka zake, Mbwana Samatta na Saimon Msuva.

Kinda huyo, alisema  amejikuta anaingiwa na shauku ya kutaka kupambana zaidi ili siku moja awe mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho cha timu ya taifa ya Tanzania.

“Kila siku nimekuwa nikijifunza na ninamshukuru sana kocha Amunike kwa kuniamini na kuniita timu ya taifa, nimejifunza vile mbinu, nidhamu na vingine vingi kutoka kwa kaka zangu
“Kilivyotangazwa kikosi cha wachezaji 23, Samatta aliniambia kwa umri wangu bado nina nafasi ya kuichezea Taifa Stars kwa hiyo sipaswi kujisikia vibaya,” alisema.

Kelvin alisema kwa namna ambavyo maandalizi yalivyo ya Taifa Stars kuna matumaini ya kufanya vizuri kwenye fainali hizo japokuwa wamepangwa kundi gumu.

“Nafasi ipo kwa timu yetu ya Tanzania kufanya vizuri,  23 waliochaguliwa watatuwakilisha vizuri, wote ni wachezaji wazuri lakini ilibidi tuwe na idadi hiyo,” alisema.

Kinda huyo wa  Kitanzania amekuwa akihusishwa kuwaniwa na klabu kadhaa barani Ulaya kutokana na kiwango alichokionyesha kwenye mashindano mbalimbali akiwa na Serengeti Boys.Miongoni mwa klabu hizo ni HB Køge ya Sweden ambayo ipo daraja la kwanza nchini humo.

Updated: 20.06.2019 14:15
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.