Kesi ya Haji Manara, wenzake kuunguruma leo

Kesi ya Haji Manara, wenzake kuunguruma leo

27 August 2019 Tuesday 13:50
Kesi ya Haji Manara, wenzake kuunguruma leo

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

KESI inayomkabiri Haji Manara na wenzake wawili inatarajiwa kuendelea tena Agosti 29, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Haji ambaye ni afisa habari wa klabu ya Simba na wenzake hao Agosti 6, 2019 walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakidaiwa deni na fidia ya milioni 83.3 baada ya kupokea bidhaa zenye nembo ya Dela Boss Perfume bila kuzilipia.

Mbali na fedha hizo, Mlalamikaji Abu Masoud Al Jahdhamy, Ameiomba mahakama kuwaamuru washtakiwa hao watatu ambao ni, Haji Manara, Beatrice Ndungu na Palm General Supply kumlipa fidia nyingine itakayoona zinafaa ikiwemo gharama za mawakili.

Kesi hiyo ya madai yenye namba 128/2019 ilitajwa kwa mara ya kwanza Agosti 6, 2019 mbele ya Hakimu mwandamizi, Wanjah Hamza.

Katika madai ya msingi, mlalamikaji amefungua kesi hiyo akiwadai walalamikiwa fedha hizo baada ya kuwasambazia bidhaa zenye nembo ya “De La Boss Perfume” Tanzania na bidhaa hizo zimetengenezwa Dubai.

PICHANI JUU:Kutoka kulia Abu Masoud Al Jahdhamy akiwa na Haji Manara, Beatrice Ndungu na  mwakilishi wa kampuni ya Palm General Supply

Updated: 29.08.2019 11:08
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.