banner68
banner58

Kiungo Yanga hoi Zanzibar

Kiungo Yanga hoi Zanzibar

31 August 2018 Friday 12:46
Kiungo Yanga hoi Zanzibar

Kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga ambaye bado hajafanikiwa kuonekana na uzi wa klabu hiyo, Mohammed Issa ‘Banka’ amefunguka kuwa kwa sasa yuko kwao Zanzibar akiuguza magoti.

Banka alisajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea Mtibwa Sugar, lakini mpaka sasa hajawahi kuonekana hata katika mazoezi ya timu yake hiyo mpya.

“Sasa hivi nipo nyumbani Zanzibar ninaumwa magoti lakini namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimekuwa nikiwasiliana na viongozi wa timu kipindi hiki.

“Yanga wanajua kama naumwa na wamekuwa wakiwasiliana na mimi vyema bila tatizo na nikipona nitaonekana tu,” alisema Banka.

Hata hivyo, taarifa ambazo siyo rasmi zilidai kuwa sababu za kutoonekana mchezaji huyo ni kutokana na kutopewa pesa zake za usajili na Yanga.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.