banner68
banner58

Kiwango duni cha Fei Toto gumzo kwa Yanga

Kiwango duni cha Fei Toto gumzo kwa Yanga

17 September 2018 Monday 12:31
Kiwango duni cha Fei Toto gumzo kwa Yanga

Katibu wa Baraza la Wazeee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema jana hakufurahishwa na ufundi wa kiungo wa timu yake, Feisal Salum 'Fei Toto' katika mchezo dhidi ya Stand United.

Akilimali ameeleza hayo baada ya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya ushindi wa mabao 4-3 na kuifikishia Yanga alama 6 ikishinda mechi zote mbili za ligi.

Katibu huyo anaamini bado kiungo kiungo huyo ataendelea kwa vizuri kwa mechi zijazo ingawa kwa jana hakufurahishwa na namna uchezaji wake ulivyokuwa.

Aidha, Akilimali ameshauri Toto kuendelea kupambana ili kujitengenezea njia za kulisongesha soka lake nje ya Tanzania ili kutimiza ndoto zake kwa uwezo alionao ndani ya Uwanja.

Toto alisajiliwa na Yanga akitokea JKU ya Zanzibar na kusaini mkataba wa miaka miwili huku usajili wake ukigubikwa na zengwe baada ya Singida United kudai walikuwa wameshamalizana naye.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.