Klabu sita Uingereza, moja Italia zamgombea Mbwana Samatta

Klabu sita Uingereza, moja Italia zamgombea Mbwana Samatta

05 June 2019 Wednesday 19:22
Klabu sita Uingereza, moja Italia zamgombea Mbwana Samatta

MSHAMBULIAJI timu ya Taifa Tanzania, Mbwana Samatta yupo mbioni kuondoka katika klabu KRC Genk baada ya Brighton na Aston Villa kuonyesha kuhitaji huduma yake.


Samatta amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwaniwa na timu za Watford, Aston Villa, Leicester na Burnley (Ligi kuu England) ambao wamemuekea Pauni 12 Milioni ambazo ni sawa na Sh35Bilioni za kitanzania.


Brighton walikuwa wakimfuatilia Samatta kwa muda mrefu huku kocha wa zamani wa timu hiyo, Chris Hughton akiwa shabiki namba moja wa mchezaji huyo, lakini pia kocha wao mpya Graham Potter naye ameonyesha kumuhitaji.

Changamoto kubwa safari hii kwa Brightoni ni kuongezeka kwa timu ambazo zimeonyesha nia ya kumuhitaji kutoka Uingereza, pia FC Roma (Italia) na Lyon (Ufaransa). 


Mshambuliaji huyu anaweza kuondoka katika kikosi cha Genk baada ya msimu uliomalizika kufanya vizuri huku akiifungia timu hiyo magoli 23 na kuiweka timu hiyo katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ubeligiji.


Msimu uliopita licha ya kufunga magoli 23, alifanikiwa kuchukua kiatu cha Ebony Shoe ambayo ni zawadi inayotolewa katika Ligi ya Ubeligiji kwa mwafrika anayefanya vizuri.


Samatta ataiongoza Tanzania katika Fainali za Afcon mwaka huu akiwa kama nahodha, huku timu hiyo ikiwa imevunja rekodi ya kufuzu baada ya kushindwa kufanya hivyo tangu mwaka 1980.

Updated: 06.06.2019 07:53
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.