KMC waanza kujifua

KMC waanza kujifua

20 June 2019 Thursday 08:46
KMC waanza kujifua

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
TIMU ya KMC inaingia kambini hii leo Juni 20,2019 kujiandaa kushiriki  mashindano ya Kagame yatakayochezwa nchini Rwanda mwezi Julai.

Msemaji wa timu hiyo, Anwar Binde amesema  kikosi cha timu hiyo kitakuwa chini ya kocha msaidizi Hamad Ally.

"Muda wowote tutamtangaza kocha mkuu wa timu lakini Juni 20, 2019 timu itaingi kambini kujiandaa na mashindano ya Kagame. Tunashiriki kama timu mwalika,'' amesema Binde

Msemaji huyo amesema pamoja na mambo mengine wataendelea kubaki na wachezaji wao na tayari baadhi wamepewa mikataba mipya.

"Japo kocha mpya tunatarajia ataongeza wachezaji wapya kulingana na mahitaji yake, lakini wachezaji wengi wa sasa tutaendelea kuwanao,'' amesema

KMC inashiriki mashindano ya Kagame kwa mara ya kwanza na ni sehemu ya maandalizi yao kujiandaa na mashindano ya shirikisho barani Afrika.

Timu ya Simba na Yanga wamejitoa kushiriki mashindano ya Kagame huku Azam ikishiriki kama bingwa mtetezi wa kombe hilo.
 
Timu ya Zesco ya Zambia na TP Mazembe ya DR Congo ni miongoni mwa timu zitakazoshiriki mashindano hayo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.