banner68
banner58

Kocha Asante Kototo azitolea macho Simba, Yanga

Kocha Asante Kototo azitolea macho Simba, Yanga

11 August 2018 Saturday 07:31
Kocha Asante Kototo azitolea macho Simba, Yanga

BONGO raha bwana kwani Kocha Mkuu wa Asante Kotoko ya Ghana, Samuel Kwasi ametamka kuwa anatamani kuja kufanya kazi na moja ya klabu nchini kutokana na kuvutiwa na mazingira ya Tanzania.

Amesema, anajua Tanzania kuna timu kubwa zenye ushindani kama Simba na Yanga hivyo anatamani kuja kufanyanya kazi hapa.

Kocha huyo ambaye ni Mghana alikuja nchini pamoja na kikosi hicho, wakacheza mechi ya kirafiki na Simba katika sherehe za Simba Day.

Amesema: "Kilichonivutia ni namna ambavyo Watanzania walivyokuwa na hamasa kwenye soka kama namna nilivyoona, nimependa na natamani sana kuja kufanya kazi hapa."

Amesema, hiyo ndiyo hamu yake kubwa na amejikuta akipenda baada ya kufika nchini.      

Katika mchezo huo uliopigwa siku ya Simba Day matokeo yalikuwa ni sare ya bao 1-1.

Updated: 11.08.2018 08:02
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.