Kocha Aussems atoa maelekezo mapya Simba

Kocha Aussems atoa maelekezo mapya Simba

25 July 2019 Thursday 14:13
Kocha Aussems atoa maelekezo mapya Simba

Rusternburg, Afrika Kusini
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ametoa maelekezo mapya na sasa  anataka kuona wachezaji wakicheza nafasi zaidi ya moja kwa sababu msimu huu anataka kuwa na mifumo miwili au mitatu ya kiuchezaji.

Ametangaza msimamo wake huo mara baada ya kumalizika mchezo wa kirafika dhidi ya Platinum Stars ambao Simba ilipata ushindi wa magoli 4-1.

“Kwasasa nataka kuona wachezaji wakicheza nafasi zaidi ya moja sababu huu msimu nataka kuwa na mifumo miwili au mitatu” amesema kocha Aussems.
Tayari kocha huyo ameshafanya mabadiliko ya  ratiba zake  za maandalizi kutoka na ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa kutoka.

Pia mabingwa hao wa Tanzania Bara, watamenyana na Power Dynamos ya Zambia Agosti 6, 2019 Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki kwenye tamasha la Simba Day.

Ratiba ya michuano ya kimataifa ya awali klabu bingwa Afrika inaonyesha kuwa Simba itacheza mchezo wake wa awali kati ya Agosti 9/10/11 na timu ya UD DO Songo ya Msumbiji.

Kocha anatoa uamuzi huo wakati tayari wachezaji John Bocco, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Aishi Manula, Hassan Dilunga, Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu wameondoka kambini  Afrika Kusini kurejea nyumbani Tanzania kujiunga na kambi ya Taifa Stars kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za CHAN  dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya.

Simba baada ya mchezo na Platinum Stars, itateremka tena uwanjani Jumamosi kumenyana na Township Rollers ya Botswana kabla ya kukamilisha ziara yake kwa kucheza na Orlando Pirates ya Johannesburg Julai 30, mechi zote zikipigwa Rusternburg.

Simba SC imelazimika kurudisha nyuma kwa siku mbili tamasha hilo ambalo kila mwaka hufanyika Agosti 8 baada ya ratiba ya Ligi Mabingwa Afrika kutoka ikionyesha mechi za kwanza za raundi ya Kwanza zitachezwa kati ya Agosti 9 na 11. 

Simba SC wataanzia ugenini dhidi ya UD do Songo ya Msumbiji kati ya Agosti 9 na 11 kabla ya kurejea nyumbani kwa mchezo wa marudiano kati ya Agosti 23 na 25.

Updated: 29.07.2019 14:25
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.