banner68
banner58

Kocha Masoud Djuma akabidhiwa mechi dhidi ya Yanga

Kocha Masoud Djuma akabidhiwa mechi dhidi ya Yanga

16 September 2018 Sunday 16:23
Kocha Masoud Djuma akabidhiwa mechi dhidi ya Yanga

BAADA ya kugundua umuhimu na ugumu wa mechi ya Yanga, Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems ameianzia mkakati maalum ikiwemo kumkabidhi majukumu mengi ya mchezo huo, msaidizi wake, Masoud Djuma.

Masoud ambaye ni mzoefu na Ligi Kuu Bara, atakuwepo kwenye Uwanja wa Taifa leo kuangalia mabadiliko ya kiufundi yaliyomo katika kikosi cha Yanga inayocheza na Stand United wakati Simba ikijiandaa kwenda Mwanza.

Simba na Yanga zimebakiza siku 14 kabla ya kupambana kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo Mnyama atakuwa mwenyeji.

Aussems ambaye timu yake ilicheza jana na Ndanda mjini Mtwara, ameliambia Spoti Xtra kwamba ameangalia mchezo wa mwisho wa watani wa jadi lakini amegundua kuna mabadiliko makubwa ya wachezaji haswa kwa Yanga ambayo anahitaji kuyafanyia kazi haraka.

Habari za uhakika zinasema kwamba Masoud hatakuwepo kwenye mechi zote za kanda ya ziwa na atalazimika kuangalia kiumakini kabisa uimara na udhaifu wa Yanga kwenye mechi ya leo na zile mbili zinazofuata dhidi ya Coastal Union na Singida.

Kulingana na taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinasema kwamba Aussems amekaa na timu yake ya ufundi akawaambia kwamba mechi hizo zitatosha kutoa picha ya mabadiliko yaliyopo ndani ya Yanga kwavile zote watatumia mbinu tofauti.

Wachezaji ambao hawapo kwa upande wa Yanga ni pamoja na Obrey Chirwa, Youthe Rostand na Hassan Kessy ambao wote walicheza mchezo ule na wapya ni Herieter Makambo, Feisal Salum, Deus Kaseke. Klaus Kindoki, Jafary Mohammed na Mrisho Ngassa.

Kwa Simba ambaye hayupo ni Laudit Mavugo ingawa kuna maingizo mapya kama Meddie Kagere, Pascal Wawa, Adam Salamba, Marcel Kaheza, Mohamed Rashid na Deogratius Munishi ‘Dida’

“Yanga ina mabadiliko, ambayo niliweza kuiona siyo kama ya sasa lakini kwangu naona hii mechi ni kama mechi nyingine sababu presha kubwa bado inabaki kwa mashabiki,”Aussem amesema.

Kocha huyo aliongeza kwamba; “Na kwa upande wa kikosi changu wachezaji wapo lakini wengine wameongezeka hivyo huwezi kufananisha na kikosi kile ambacho kiliweza kucheza msimu ule.” Masoud alionekana akichukua dondoo kwenye mechi ya African Lyon na Coastal Union na alipoulizwa alisisitiza alikuwa akifanya tathmini ya washindani wake kama sehemu ya kazi ya benchi lake ya ufundi ingawa hakutaka kufafanua zaidi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.