banner68
banner58

Kocha Masoud Djuma mbioni kujiunga Yanga

Kocha Masoud Djuma mbioni kujiunga Yanga

03 September 2018 Monday 09:16
Kocha Masoud Djuma mbioni kujiunga Yanga

Yanga wanafikiria kumpa ofa Kocha mwenye mbwembwe mazoezini, Masoud Djuma kama Simba wakikubaliana kumpiga chini.

Lakini Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye mpaka sasa hana msaidizi, jana Jumamosi akiwa Liberia ametanabaisha kuwa anamjua Djuma na akiletewa atafanya nae kazi vizuri kwa vile ni mzoefu.

Habari za ndani ya Simba zinasema kwamba uongozi uko kwenye mchakato wa kumuondoa Djuma kwa kile kilichoelezwa kwamba picha haziivi na bosi wake, Mbelgiji Patrick Aussems ambaye inadaiwa amewabonyeza viongozi wampige chini.

“Sina tatizo lolote kikubwa ni kufuata utaratibu tu wa kazi ambao yeye kama kocha anaujua, kwa hiyo kama itatokea ikawa hivyo mimi sina tatizo nitafanya naye kazi,” alisema Zahera ambaye Msaidizi wake, Shadrack Nsajigwa alijiuzuru kukwepa presha na lawama za mashabiki.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema kwamba baadhi ya viongozi wameanza kujadiliana uwezekano wa kumpa ofa kocha huyo ingawa wengine wanapinga, licha ya kwamba Haji Manara amekuwa akisisitiza kwamba Djuma haondoki.

Wanaopendekeza achukuliwe wanadai kwamba Djuma ana uwezo wa kujenga morali na ndiye anayefanya kazi kubwa ndani ya Simba kwa sasa licha ya wengi kumuangalia Mbelgiji.

Lakini vigogo wengine ndani ya Yanga wanaopinga waziwazi wazo hilo wanadai kwamba Kocha huyo ana Usimba na ameshatengeneza mtandao mkubwa Msimbazi hivyo itakuwa ngumu kufanya kazi kwa moyo Yanga.

Lakini Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Yanga, Hussein Nyika alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo jana alizuga na kusisitiza kwamba bado wanaendelea na mchakato wa kutafuta msaidizi wa Zahera.

Djuma jana hakutoa ushirikiano kuhusiana na hatma yake ndani ya Simba lakini Spoti Xtra lilidokezwa kwamba jioni alikuwa na kikao na baadhi ya vigogo wa Msimbazi ambacho moja ya vitu ni kuzungumzia ishu ya kumpiga chini.

Lakini mjadala huenda ukaibuka kwenye ishu ya mkwanja kwani Djuma kwa sasa analipwa Sh.Mil.13.6 Simba akiwa kama Kocha Msaidizi ambazo ni nyingi kuliko Zahera ambaye Yanga wanamlipa Sh.Mil.6.8.

Updated: 03.09.2018 09:24
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Ben mapogo 2018-09-03 11:29:23

Ni bora angalie mahala pakufanya kazi kuliko kunyanyaswa! masoud yanga panakufaa sana njoo ufanye kazi

Avatar
Daimoni wiliam 2018-09-12 13:27:48

Masud djuma nikocha mwenye sifii akiwa natimu kwani uwezo wake ni wahali ya juu mno afananishwi na kocha wa TPL TANZANIA.

Avatar
Rogatustawete@gmail.com 2018-09-14 16:36:58

Bora upate timu Ya kufanya kazi kuliko manyanyaso mengi Wew Bonge LA kocha masoud djuma

Avatar
niete shabick wa kwel ELIVINIUS DEOGRATIAS{xponxor} kocha hana utimu kwan anatafuta 2 kazi ila kwa shwara la ngassa asiwe anatolewa labda MAKAMBO ndo awe anatolewa hana pumzi 2018-09-17 12:23:19

yanga damu ila sijapend kumtoa ngassa na ajibu huku wakimuacha makambo pamoja na kipa

Avatar
Wambura shoferi 2018-09-17 16:52:48

Djumaa tunakukaribisha yanga kama unapenda njoo,karibu san.

Avatar
saidi juma 2018-09-20 01:34:16

kiukweli sisi mashabiki wa simba tunakukubali sana djuma ila ubinafsi na kutotoa ushirikiano kwa kocha,mkuu ndo unazingua bhana simba nikubwa kuliko masoud djuma, jaman,

Avatar
salum matola 2018-09-21 13:53:36

Mm binafsi kama mshabiki wayanga timu yetu inashinda lakini kiukweli eneo LA ulizi alipo vizur pamoja eneo laushambuliaji alikovizuli

Avatar
Moshi Likungwa 2018-09-25 07:29:47

Masoud Njoo Jangwan Chama La Wananch Karb Ss Tushakua Watam Apa Fei Toto Ap Tshishimbi Uku Ngasa Kaseke Ajib Muhuaj Makambo Wote Haw Watakupa Heshma Yko Masoud Djumaa Njoo.