banner68
banner58

Kocha Mwinyi Zahera aanza maandalizi ya kuiua Simba

Kocha Mwinyi Zahera aanza maandalizi ya kuiua Simba

16 September 2018 Sunday 16:28
Kocha Mwinyi Zahera aanza maandalizi ya kuiua Simba

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, anajua kwamba mechi yake itakayoikutanisha timu yake dhidi ya watani wao wa jadi, Simba ni muhimu sana kwa ustawi wa kibarua chake hapo Jangwani, hivyo alichofanya ni kuhakikisha anashirikiana na uongozi kupanga mikakati ya ushindi wa mechi hiyo pamoja na ubingwa.

Raia huyo wa DRC alirejea nchini wiki hii akitokea kwao alikokwenda kwa ajili ya kuitumikia timu yake ya Taifa iliyokuwa ikicheza na Libya katika mechi ya kufuzu michuano ya Afcon.

Lakini kabla ya kwenda huko, imefahamika kuwa, aliposaini tu mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo alianza kuangalia kikosi kilichosajiliwa na kupima kila aina ya mchezaji na kuridhishwa na viwango vyao.

Baadaye alifarijika baada ya uongozi wa klabu huyo kupata saini ya Straika Heritier Makambo, ambaye tayari hadi sasa ameshaipachikia timu yake bao moja katika michuano ya Ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kazi yake ya pili aliyoifanya ni kuichungulia ratiba ya Ligi Kuu iliyoanza Agosti 22, ili kuona idadi ya mechi ambazo zitamhakikishia pointi.

Hatimaye mpango huo sasa umeiva na hivi jana tu kocha huyo akielezea mchezo wao wa leo dhidi ya Stand United, utakuwa maalumu kwa kuanza safari yao ya kurejesha ubingwa wao.

Yanga itacheza mechi 11 katika Uwanja wa Taifa, kati ya hiyo saba itakuwa wenyeji na nne itakuwa ugenini, lakini itachezwa Uwanja wa Taifa, kutokana na timu itakazocheza nazo pia kutumia uwanja huo.

Michezo ambayo watacheza Yanga mfululizo Uwanja wa Taifa ni Yanga vs Stand United, Yanga  vs Coastal Union, Yanga vs Singida United, JKT Tanzania vs Yanga, Simba vs Yanga, Yanga vs Mbao FC, Yanga  vs Alliance FC, KMC FC vs Yanga,
Yanga  vs Lipuli FC, Yanga  vs Ndanda FC, African Lyon vs Yanga.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussein Nyika, alisema kuanza nyumbani mechi nyingi kwao ni faida, hivyo wanatakiwa kupambana kama askari kuhakikisha wanachukua pointi za michezo yote 11 watakayochezea Uwanja wa Taifa.

“Hii ni fursa, bali na mapambano kucheza kama fainali kwa kila mechi, ili kufaidika na ratiba jinsi ilivyo,” alisema Nyika.

Alisema hesabu zao msimu huu ni kuchukua ubingwa mapema, hivyo ni lazima wapambane sana na kutumia vizuri nafasi watakazozipata.

“Tuna kikosi imara, na pia tutalitumia dirisha dogo la usajili kuboresha kila idara ambayo mwalimu wetu ataona lina mapungufu ili tuweza kupambana na vita iliyopo mbele yetu,” alisema Nyika.

Yanga wamecheza mechi moja ya ligi mpaka sasa dhidi ya Mtibwa Sugar na kufanikiwa kutoka na pointi 3, baada ya kuwafunga mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.