banner68
banner58

Kocha Ndanda FC atuma salamu kwa Patrick Asseums

Kocha Ndanda FC atuma salamu kwa Patrick Asseums

15 September 2018 Saturday 07:28
Kocha Ndanda FC atuma salamu kwa Patrick Asseums

Kocha Mkuu wa klabu ya Ndanda, Malale Hamsini, amesema maandalizi yao kuelekea mechi ya leo dhdii ya Simba yameshakamilika.

Hamisini amesema kwa sasa wanasubiria mchezo huo utakaoanza majira ya saa 10 jioni ili waweze kuwaonesha maajabu Simba.

Kocha huyo amewakamia Simba akijiamini kuwa anaweza kuivunja rekodi ya kutokupata matokeo wanapokutana na timu hiyo kongwe kutoka mitaa ya Ilala, Kariakoo, Dar es Salaam.

Ikumbukwe tangu Ndanda ipande Ligi Kuu mwaka 2014 haijawahi kupata matokeo mbele ya Simba hata kwenye Uwanja wake wa nyumbani 'Nangwanda Sijaona'.

Kuelekea mechi hiyo, tayari wekundu wa Msimbazi wameshawasili mjini humo tangu juzi kwa ajili ya kibarua hicho cha kuwania alama tatu.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.