Kocha Patrick Aussems abadili program ya mazoezi Simba

Kocha Patrick Aussems abadili program ya mazoezi Simba

22 July 2019 Monday 16:35
Kocha Patrick Aussems abadili program ya mazoezi Simba

Na mwadishi wetu, Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema  kutokana na ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa kutoka ni lazima afanye mabadiliko kwenye ratiba zake za maandalizi.

Ratiba ya michuano ya kimataifa ya awali inaonyesha kuwa Simba itacheza mchezo wake wa awali kati ya Agosti 9/10/11 na timu ya UD DO Songo ya Msumbiji.

"Mchezo huu ni muhimu sana tunatakiwa kubadili kidogo programu yetu sababu tunatakiwa kuwa tayari kwa hiyo michezo miwili. 

"Hatukutarajia haya kabla hivyo imekuwa mshangao kwetu hatukutarajia iwe hivi ila hamna namna, tunahitaji kubadili ratiba yetu ili kuwa tayari kwa michuano mikubwa," amesema.

Simba imeweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 23.

Katua hatua nyingeni kocha Patrick Aussems  leo amemtambulisha rasmi kwa wachezaji Mtaalamu wa Tiba ya Viungo, Paulo Gomez Dardenne ambaye amejiunga na timu  kambini nchini Afrika Kusini.

Updated: 25.07.2019 13:37
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.