Kombe la Dunia 2018: Messi ampa ulaji golikipa wa Iceland

Ni baada ya kupangua mkwaju wa penati wa Lionel Messi kwenye kombe la dunia

Kombe la Dunia 2018: Messi ampa ulaji golikipa wa Iceland

Ni baada ya kupangua mkwaju wa penati wa Lionel Messi kwenye kombe la dunia

18 June 2018 Monday 13:09
Kombe la Dunia 2018: Messi ampa ulaji golikipa wa Iceland

Mlinda Mlango wa Timu ya Taifa ya Iceland inayoshiriki Kombe la Dunia Huko Russia Hannes Halldorsson ambaye alifanikiwa kudaka penati iliyopigwa na mshambuliaji Lionel Messi wa timu ya taifa ya Argentina ameahidiwa na kampuni ya SAGA FILM Kuwa atapata kazi mara baada tu ya kuachana na soka.

Golikipa huyo ambaye ana umri wa miaka 34, aliufuta mkwaju huo wa mechi ya kundi D Jumamosi na kuishangaza Dunia kutokana na umakini wake alipokuwa uwanjani kwa kuokoa michomo mingi iliyokuwa ikielekezwa langoni mwake.

Kipa huyo kwa sasa anakipiga katika klabu ya Randers FC Inayoshiriki ligi kuu nchini Denmark na huwa anajishughulisha na uongozaji wa filamu wakati wa likizo na alipokuwa na umri mdogo alikuwa akipenda sana kupiga picha picha na kuongoza utengenezaji wa video mbalimbali.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuwafanya Argentina kushika nafasi ya 3, nafasi moja juu ya Nigeria iliyo katika nafasi ya 4 baada ya kuchapwa 2-0 na Croatia.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.