Kufuzu Afcon 2021 Stars kukutana na timu hizi

Kufuzu Afcon 2021 Stars kukutana na timu hizi

10 July 2019 Wednesday 15:15
Kufuzu Afcon 2021 Stars kukutana na timu hizi

na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MASHINDANO ya kuwania tiketi ya kufuzu Afcon 2021, Tanzania imepangwa katika chungu cha tatu pamoja na Madagascar, Zimbabwe, Central Africa Republic (CAR), Namibia, Sierra Leone, Msumbiji, Guinea Bissau, Angola, Malawi, Togo, na Sudan.

Nchi hizi zimepangwa katika vyungu vitano kwa kuangalia orodha ya viwango vya ubora wa FIFA iliyotoka Juni 14, 2019. 

Cameroon itakuwa mwenyeji fainali hizo za 2021, ikiwa ni mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo 1972 (miaka 49 iliyopita).

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litafanya mkutano mkuu Julai 18 katika Ukumbi wa Aida Ballroom, wa Hoteli ya Marriott, Cairo, Misri na moja ya ajenda ni kupanga ratiba ya kusaka kufuzu kwa AFCON ya Cameroon 2021.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.