Kwa Yanga hii tema mate chini, washusha kifaa kipya

Kwa Yanga hii tema mate chini, washusha kifaa kipya

09 June 2018 Saturday 13:59
Kwa Yanga hii tema mate chini, washusha kifaa kipya

Na Mwandishi wetu

Wakati chama cha soka nchini TFF wakitoa masaa 48 kwa Yanga kutengua kauli yao ya kujitoa katika michuano ya Kagame huku wakiwaeleza madhara yatakayoikumba timu hiyo endapo watawasilisha barua yao CECAFA, timu hiyo ya mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam wameamua kufanya kweli katika usajili wa wachezaji kuelekea msimu mpya wa soka nchini.

Leo hii tayari wameshusha kifaa kitakachovaa jezi namba 11 aliyoiacha Donald Ngoma kutoka Benin.

Marcelin Koukpo ambaye alikuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na uongozi wa Yanga ametua leo tayari kusaini mkataba na mabingwa hao mara 27 wa ligi kuu nchini.

Mchezaji huyo aliwahi kucheza Les Buffles FC ya huko Benin inaelezwa tayari ameshamalizana kwa kila kitu na Yanga na atasaini mkataba wa miaka miwili.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.