Laliga: Athletic Bilbao yainyamanzisha Barcelona

Laliga: Athletic Bilbao yainyamanzisha Barcelona

17 August 2019 Saturday 06:50
Laliga: Athletic Bilbao yainyamanzisha Barcelona

PAZIA la ligi kuu ya Hispania(Laliga) imefunguliwa usiku wa kuamkia leo kwa Barcelona kufungwa goli 1-0 na timu ya Athletic Bilbao.

Goli la dakika za lala salama(dakika 89) lililofungwa na mshambuliaji mkongwe Aritz Aduriz ndio limeiwezesha timu hiyo kuchukua point tatu muhimu na kuongoza ligi kwa muda.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 38 anaweka historia kwa kuwa mchezaji aliyefunga goli la kwanza la ufunguzi pia alifunga goli hilo ikiwa ni dakika moja baada ya kuingia uwanjani. Aliingia kunako dakika ya 88

Bilbao wakiwa katika uwanja wake wa nyumbani imewaduwaza wachambuzi na mashabiki wa soka ambao wengi waliipa nafasi ya ushindi Barcelona katika mechi hiyo ya ufunguzi

Barcelona inakuwa timu ya kwanza kuanza na kipigo LaLiga na kuiacha Bilbao ikiongoza Ligi kwa muda

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.