Laliga: Barcelona yafungwa

Laliga: Barcelona yafungwa

22 September 2019 Sunday 06:11
Laliga: Barcelona yafungwa

KLABU ya FC Barcelona ya Hispania usiku wa kuamkia Septemba 22, 2019 imejikuta ikipata kipigo cha pili katika ligi kuu ya Hispania maarufu Laliga msimu wa mwaka 2019/20 baada ya kufungwa goli 2-0 na timu ya Granada.

Wakiwa ugenini Barcelona walianza kufungwa goli la kwanza kunako dakika ya 2 na Ramon Azeez na kunako dakika 66 mchezaji Alvaro Vadillo aliiandikia timu yake hiyo goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya kiungo Arturo Vidal wa Barcelona kusababisha penati akitokea benchi.

Mechi hiyo ambayo nahodha wa Barcelona Lionel Messi aliingia kipindi cha pili akitokea benchi haikuwa rahisi tofauti na matarajio ya wachambuzi na mashabiki wengi wa soka duniani .

Ushindi huo wa Granada unawafanya wafikishe jumla ya point 10 na kukaa kileleni mwa msimamo wa LaLiga kwa tofauti ya magoli ya kushinda na kufungwa dhidi ya timu ya Sevilla na Atletico Madrid wanazolingana kwa kuwa na point 10 kila timu.

Baada ya kupoteza katika mchezo huo wa ugenini Barcelona wanaendelea na rekodi yao ya kutopata ushindi LaLiga ugenini tangu April, 2019.

MATOKEO KAMILI HAYA HAPA:

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.