Lechantree kutupiwa virago Simba, Masudi Djuma kuwa kocha mkuu

Adaiwa kushindwa kuifikisha timu hiyo kwenye uwezo uliotarajiwa

Lechantree kutupiwa virago Simba, Masudi Djuma kuwa kocha mkuu

Adaiwa kushindwa kuifikisha timu hiyo kwenye uwezo uliotarajiwa

06 June 2018 Wednesday 14:49
Lechantree kutupiwa virago Simba, Masudi Djuma kuwa kocha mkuu

Na Amini Nyaungo

Kama ulikuwa hujui siku 43 zimebaki kabla mkataba wa kocha mkuu wa Simba Pierre Lechantree kumalizika muda wake ndani ya klabu hiyo.

Lechantree  ambaye ameiwezesha klabu hiyo ya Msimbazi kubeba taji la ligi kuu Tanzania Bara baada ya kulikosa kwa miaka mitano, alichukua nafasi ya kocha wa zamani raia wa Cameroon Joseph Omog.

Taarifa ambazo bado hazijathbitishwa zinasema, kocha huyo atafungashiwa virago vyake baada ya kushindwa kufikia uwezo uliotegemewa na uongozi wa klabu hiyo baada ya kumpa kazi ya kukinoa kikosi cha timu hiyo kubwa nchini.

Kinachoelezwa kocha huyo hajabadilisha kitu ametumia mfumo wa Masudi Djuma na hakuweza kuifikia rekodi ya Joseph Omog ambayo mzunguko wa kwanza timu hiyo imeenda bila kufungwa na kutoa sare moja pekee.

Haji Manara akiwa Kenya amethibitisha kwamba mkataba wa kocha wao unaelekea ukingoni na amewaomba wanasimba kuwa watulivu na wavumilivu wakisubiri uongozi uamue kama utaendelea au utaachana na kocha huyo.

“Kocha Lechantre mkataba wake unamalizika mwezi hivi karibuni uongozi utakaa nae utaona kama ipo haja ya kuendelea nae au la” alisema Haji Manara.

Utata

Inaonekana kuna utata ndani yake kati ya kocha msaidizi Masudi Djuma na Lichantree katika upangaji wa timu.

Pia kocha huyo siku hizi haonekani akisimama kama ilivyokuwa siku za nyuma wakati wa mechi ikiendelea. Inasemekana kuna bifu zito na kocha huyo ambaye inaelezwa kuwa hataki kubadilika.

Unajua Simba wanawaza nini?

Masudi Juma ndiye kocha atakayechukua mikoba ya Lichantree baada ya kuisha mkataba wake, taarifa zinazoenea kuwa Masudi Djuma anaweza kuondoka hazina ukweli wowote na inaonekana tayari ameshaongea na uongozi na atakula shavu kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Azania Post

Updated: 06.06.2018 15:00
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.