Lichantree aondoka, amesema nidhamu hakuna Simba

Lichantree aondoka, amesema nidhamu hakuna Simba

14 June 2018 Thursday 12:57
Lichantree aondoka, amesema nidhamu hakuna Simba

Na Amini Nyaungo

Huenda ikawa hujui ila ndio hivyo tena uhusiano wa Pierre Lechantre na Simba ndiyo umefikia ukingoni siku ya Jumatano, hivi sasa kocha huyo anasubiria sikukuu ya Eid al Fitr nchini kwao Ufaransa.

Kocha huyo alikuwa anasubiria tuzo za Mo Awards ambazo zimefanyika siku ya Jumapili na kuteka hisia za watu wengi Tanzania.

Lechantre ameacha wosia mzito katika klabu hiyo huku kubwa likiwa ni nidhamu ya wachezaji akisema haikuwa nzuri hata kidogo.

Lechantree alisaini mkataba wa muda mfupi kulingana na matakwa ya viongozi wa Simba ambapo waliona hawezi kuivusha Simba kuelekea kisiwa cha ahadi ambayo mashabiki na wapenzi wengi wa timu hiyo wanatamani timu hiyo ifike huko katika mafanikio.

Lechantree ambaye ni raia wa Ufaransa moja ya makocha wenye historia kubwa Barani Afrika aliyoipata akiwa nchini Cameroon.

Hivi sasa timu hiyo ipo mikononi mwa Mrundi Masoud Djuma na inawezekana akachukua moja kwa moja mikoba ya kuwanoa mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania Bara na kuwa kocha mkuu kulingana na taarifa za ndani za timu hiyo.

Kocha huyo amesema changamoto kubwa aliyoipata ni pamoja na mazingira ya viwanja vya nchini kuwa vibovu lakini anashuruku wameweza kuchukua ubingwa ambapo ilikuwa kiu kubwa kwa mashabiki wa Simba.

Amesisitiza kuwa nidhamu ilikuwa tatizo kubwa sana katika klabu hiyo na ndio maana amefanya jitihada hadi kufika hapo ilipofika.

Azania Post

Updated: 14.06.2018 13:03
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Hamisi Kimwaga 2018-06-14 15:07:41

Tunamshukuru japo kwa hicho kidogo alichotuachia