Ligi kuu bara kuanza Agosti 23, Simba vs Yanga Januari 4

Ligi kuu bara kuanza Agosti 23, Simba vs Yanga Januari 4

08 July 2019 Monday 14:51
Ligi kuu bara kuanza Agosti 23, Simba vs Yanga Januari 4

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
BODI ya Ligi nchini imetangaza ratiba ya Ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 ambapo Agosti 23, 2019 pazia litafunguliwa rasmi kwa mchezo mmoja kati ya Simba SC na JKT Tanzania 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura leo Julai 8, 2019 akitangaza ratiba hiyo amesema mechi itakayofuata itakuwa ni Agosti 24 kati ya Mbao Fc na Aliace zote za jijini Mwanza huku mechi ya kwanza ya watani wa jadi Yanga na Simba itachezwa  Januari 4, 2020.

Wambura amesema wiki moja kabla ya mchezo huo utapigwa mchezo wa Ngao ya Jamii ambao huwakutanisha Mabingwa wa Ligi ambao ni Simba na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho ambao ni Azam FC. Mchezo huo utapigwa Agosti 17, 2019.

"Msimu huu tumezingatia ratiba zote za kimataifa na hatutarajii mabadiliko ya ratiba kwa sababu zizisokuwa za msingi", amesema Wambura.

Timu ya Simba ndio bingwa mtetezi wa ligi hiyo yenye timu 20

Updated: 09.07.2019 08:16
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.