Lionel Messi aweka rekodi nyingine tena

Lionel Messi aweka rekodi nyingine tena

12 June 2019 Wednesday 08:45
Lionel Messi aweka rekodi nyingine tena

MSHAMBULIAJI wa Barcelona na Argentina Lionel Messi ndiye anayelipwa malipo ya juu zaidi kuliko wachezaji wote duniani , alilipwa dola milioni 127 katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, kwa mujibu wa orodha ya jarida la Forbes ya wachezaji 100 wanaolipwa vizuri.

Mshambuliaji wa Juventus, Mreno Cristiano Ronaldo anashikilia nafasi ya pili akilipwa dola milioni 109, huku mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar ambaye ni raia wa Brazil akija katiika nafasi ya tatu kwa malipo ya dola milioni 105.

Mwaka jana mchezaji aliyelipwa kuliko wote duniani alikuwa ni mwanamasumbwi Floyd Mayweather, lakini sasa ameshuka katika orodha hiyo.

Mchezaji tenesi Serena Williams ni mwanamke pekee katika watu 100 ,wanaolipwa vizuri, na kwa mujibu wa Forbes analipwa dola milioni 29.2

Mshindi wa mara tano wa mashindano ya dunia ya magari ya Formula 1 Lewis Hamilton na mshindi wa zamani wa masumbwi uzani wa juu Anthony Joshua ndio wanariadha wanaolipwa vizuri zaidi nchini Uingereza , wakichukua namba 13 na malipo ya dola milioni 55.

Jarida hilo la Marekani lilikokotoa malipo ya wanariadha kwa kujumlisha fedha za malipo ya tuzo , mishahara na nembo walizoidhinisha kati ya Juni 2018 na Juni 2019.

Miongoni mwa wanariadha wanaoshikilia nafasi za juu katika 100 kutoka nchi 25 na mapatp yao ya dola bilioni 4 yakijumlishwa yanajumuisha 5% ya kutoka mwaka jana, wakati Mayweather alipokuwa wa kwanza na malipo ya dola milioni 285.

Mpambano pekee wa bondia huyo wa Marekani tangu Agosti 2017 ulikuwa baina yake na Mjapani Tenshin Nasukawa uliofanyika Disemba.

Wanariadha walitakiwa kulipwa dola milioni 25 kuweza kuingia katika orodha Forbes ya mwaka huu.

Messi ndie mchezaji pekee wa pili wa soka kuwa juu katika viwango baada ya Ronaldo, na ndiye mwanariadha wa nane pekee miongoni mwa wanariadha tofauti kuchukua namna moja tangu orodha hiyo ilipoanza kutolewa mnamo 1990.

Ni mara ya kwanza kwa mchezaji wa mpira wa miguu kuwekwa miongoni mwa watu watatu wanaolipwa vizuri kwa kucheza.

Messi ni miongoni mwa wanamichezo 38 wasio Wamarekani kwenye orodha , huku wanamichezo nyota 62 wa Marekani wakishikilia nafasi za kwanza katika orodha ya watu 100.

Shirikisho la mchezo wa kikapu Marekani NBA ndilo lililoongoza kwa kuwa na wachezaji wengi kwenye orodha hiyo, liliwa na wachezaji 35, huku LeBron James wa LA Lakers akiwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi ambapo anashikilia nafasi ya eighth akilipwa dola 89 akija mbele ya Wachezaji wawili nyota wa Golden State Warriors Stephen Curry anayeshikilia namna 9 akilipwa dola milioni 79.8 na Kevin Durant ambaye anashililia nafasi ya 10 akilipwa dola milioni 65.4

Mchezaji wa Manchester United Paul Pogba ndiye mchezaji anayelipwa zaidi katika primia Ligi, na katika orodha ya Forbes anashikilia nafasi ya 44t na malipo ya dola milioni 33. (£25.9m).

10 walio juu katika Orodha ya Forbes:

1. Lionel Messi dola 127

2. Cristiano Ronaldo dola 109

3. Neymar dola milioni 105

4. Canelo Alvarez dola milioni 94

5. Roger Federer dola milioni 93.4

6. Russell Wilson dola milioni 89.5

7. Aaron Rodgers dola milioni 89.3

8. LeBron James dola milioni 89

9. Stephen Curry dola milioni 79.8

10, Kevin Durant dola milioni 65.4

Updated: 12.06.2019 17:25
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.