Liverpool bingwa mpya Uefa Super Cup

Liverpool bingwa mpya Uefa Super Cup

15 August 2019 Thursday 05:10
Liverpool bingwa mpya  Uefa Super Cup

TIMU ya Liverpool imefanikiwa kuchukua ubingwa wa kombe la Uefa Super Cup baada ya kuifunga Chelsea kwa penati.

Mabingwa hao wa ligi ya mabingwa Ulaya imekabiliana na upinzani mkali kutoka  kwa Chelsea katika mchezo uliochezwa nchini Ituruki na kutoshana nguvu ya goli 2-2 katika dakika zote za  mchezo huo .

Lakini kupitia mikwaju ya penati Liverpool imepata penati zote tano na Chelsea imepata penati nne na kupoteza moja.

Kunako dakika 36 kipindi cha kwanza mshambuliaji wa Chelsea Oliver Giround aliiadikia timu yake hiyo goli la kuongoza.

Sadio Mane wa Liverpool alisawazisha goli hilo kunako dakika ya 48. Dakika ya 95 Mane aliingia kambani tena lakini kiungo wa Chelsea Jorginho kunako dakika 101 za nyongeza alisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati .

Mpambano huo unakuwa ni wa mara ya kwanza kwa timu za Uingereza kukutana katika historia ya kombe hilo.

Kombe la Super Cup limebebwa sana na klabu za Hispania hali ya kwamba limepata makazi mapya nchini humo katika siku za hivi karibuni huku washindi watano wa kombe hilo wote wakitoka Hispania.

Lakini kombe hilo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14 limeelekea Uingereza mwaka huu huku mechi hii ikiwa ya kwanza kupiganiwa kati ya timu mbili za ligi ya Premia.

Kwa jumla fainali saba za kombe la Super Cup zimekuwa kati ya wapinzani kutoka Hispania ikiwemo timu nne tangu 2014 na timu mbili zote kutoka Itali.

Updated: 15.08.2019 06:15
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.