Liverpool yaanza kwa ushindi mnono EPL

Liverpool yaanza kwa ushindi mnono EPL

10 August 2019 Saturday 07:09
Liverpool yaanza kwa ushindi mnono EPL

Liverpool, Uingereza
LIVERPOOL imeanza msimu wa ligi mwaka 2019/20 wa EPL kwa ushindi mnono wa magoli 4-1 katika mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Anfield  dhidi ya Norwich City.

Goli la kwanza la Liverpool lilipatikana dakika ya kwanza tu kwa mchezaji wa Norwich, Hanley kujifunga, dakika ya 19 Mohammed Salah alipachika, Van Dijk dakika ya 28 na Divock Origi akafunga goli la nne dakika ya 42 huku kunako dakika ya 64 Pukki alifunga goli la kufuatia machozi kwa Norwich.

Ushindi huo umeanza kwa kuipa baraka Liverpool ya kuwa timu ya kwanza kuanza kukaa kileleni mwa msimamo wa EPL kabla ya timu nyingine 18 kucheza, msimu uliopita Liverpool walipoteza nafasi ya kutwaa Ubingwa kwa tofauti ya alama moja dhidi ya Man City.

Updated: 10.08.2019 07:21
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.