banner68
banner58

Lwandamina aenda na mzimu wa Yanga Zesco United

Timu yake mpya ya Zesco United yapokea kichapo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika

Lwandamina aenda na mzimu wa Yanga Zesco United

Timu yake mpya ya Zesco United yapokea kichapo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika

17 May 2018 Thursday 14:04
Lwandamina aenda na mzimu wa Yanga Zesco United

Na Amini nyaungo

Baada ya kuondoka aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina kama ameacha majanga katika klabu hiyo maana haijashinda hata mechi moja.

Sasa naye hapo jana imeanza vibaya na timu yake mpya Zesco United katika ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Etoile Sahel timu kutoka Tunisia imeweza kuichabanga mabao 2-1 katika hatua ya makundi katika kundi D.

Katika mchezo wa kwanza Zesco United ilitoa sare 1-1 dhidi ya Swallows.

Hii imekuwa kama mwendelezo wa timu yake ya zamani Yanga kufanya vibaya katika michuano ya nje na ndani naye amepokea kijiti hicho akipokea kipigo.

Kwa matokeo hayo yanawafanya mabingwa hao wa zamani wa Afrika, Etoile kuuungana na Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye usukani wa kuongoza kundi hilo la D ikiwa timu zote zimejikusanyia alama nne.

Wakati klabu ya Zesco United ikiangukia nafasi ya tatu huku Primeiro Agosto ya Angola ikiburuza mkia.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.