Maajabu ya Barcelona Kombe la Dunia 2018

Maajabu hayo ni pamoja na timu hiyo kutoa wachezaji katika makundi yote katika fainai hizo

Maajabu ya Barcelona Kombe la Dunia 2018

Maajabu hayo ni pamoja na timu hiyo kutoa wachezaji katika makundi yote katika fainai hizo

05 June 2018 Tuesday 11:48
Maajabu ya Barcelona Kombe la Dunia 2018

Na Amini Nyaungo

Kuelekea kombe la dunia mwaka 2018, leo zimesalia siku 9 hadi fainali hizo kuanza kutimua vumbi katika miji mbalimbali nchini Urusi. Yapo mengi ambayo yameandikwa, lakini inawezekana hufahamu maajabu kwa mabingwa wa soka nchini Hispania, yaani Barcelona.

Huenda haijawahi kutokea hii mara nyingi timu za Uingereza ndio zinatoa wachezaji wengi lakini Barcelona imeweza kuweka rekodi nyingine kubwa.

Maajabu hayo ni pamoja na timu hiyo kutoa wachezaji katika makundi yote katika fainai hizo, yaani kuanzia kundi ‘A’ hadi ‘H’.

Kundi ‘A’ ambao lina timu ya Taifa ya Uruguay. Huyu ndiyo staa wa timu hii ya Amerika ya Kusini na tegemeo kubwa kwa timu yake katika mbio za kulisaka kombe hilo baada ya miaka mingi bila kulibeba. Kundi hili lina timu nyingine tatu, ambazo ni Urusi,Saudia Arabia na Misri.

Kundi ‘B’ambalo lina timu ya taifa ya Hispania, Ureno, Morocco na Iran kuna wachezaji Gerard Pique, Jordi Alba na Sergio Busquets wote wapo timu ya taifa ya Hispania.

Kundi ‘C’ ambalo pia linaundwa na mataifa ya Denmark, Ufaransa, Australia na Peru kuna wachezaji wawili wa taifa la Ufaransa Samuel Umtiti na Ousmane Dembele.

Kundi ‘D’ lina wachezaji wawili Lionel Messi ambaye anacheza timu ya taifa ya Argentina na Ivan Rakitic wa Croatia. Kundi hili linaundwa na timu za Argentina, Croatia, Nigeria na Iceland.

Wakati kundi ‘E’ linaundwa na Brazil, Serbia, Uswisi na Costa Rica, kundi hili lina wachezaji wawili wa Barcelona Phillipe Coutinho na Paulinho.

Kundi ‘F’ lina mchezaji mmoja ambaye ni golikipa wa Barcelona Andre Ter Stegen wa timu ya taifa ya Ujerumani kundi hili linaundwa na Ujerumani, Mexico, Sweden na Korea Kusini.

Kundi ‘G’ kuna mchezaji mmoja Thomas Vermalen wa taifa la Ubelgiji wakati kundi hili huundwa na Ubelgiji, Panama, Tunisia na Uingereza.

Kundi ‘H’ ambalo ndilo la mwisho pia kuna mchezaji mmoja Yeri Mina wa Colombia, huku kundi hili linaundwa na Colombia, Senegal, Japan na Poland.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Betting Tips 2018-06-13 12:52:34

Usikose nafasi hii ya kujishindia simu ya Techno WX3. Bashiri katika mechi za kombe la Dunia na PMbet na ujaribu bahati yako. https://pmbet.co.tz/en/home

Avatar
Betting Tips 2018-06-14 12:05:48

Bashiri na PMbet katika kombe la Dunia 2018