Magoli 21 yamefungwa kombe la dunia: Ronaldo aongoza kwa ufungaji bora

La Liga yaongoza miongoni mwa wafungaji kwenye Kombe la Dunia

Magoli 21 yamefungwa kombe la dunia: Ronaldo aongoza kwa ufungaji bora

La Liga yaongoza miongoni mwa wafungaji kwenye Kombe la Dunia

17 June 2018 Sunday 12:19
Magoli 21 yamefungwa kombe la dunia: Ronaldo aongoza kwa ufungaji bora

Na Amini Nyaungo

Michuano ya kombe la dunia imeendelea kuchanja mbunga timu nne za Afrika zikiwa timepoteza zimepoteza michezo yao na Senegal ikiwa imesalia kubeba matumaini ya bara hilo wakati wa mchezo wake wa Jumanne dhidi ya Poland.

Huenda timu hiyo ya Afrika Magharibi, ikiongozwa na mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane itawatoa kimasomaso Waafrika kwa kupata ushindi na kuleta heshima huku taifa hilo likiwa katika matumaini ya kusalia katika michuano hiyo.

Baada ya kuangalia timu ya Manchester City kuwa na wachezaji wengi kombe la dunia, sasa tuangalie ligi ipi imetoa wafungaji bora hadi sasa.

Ikiwa magoli 21 yamefungwa huku Ligi Kuu ya Hipania imetoa wafungaji bora hadi sasa ikiongozwa na Cristiano Ronaldo aliye na magoli matatu na ndiye anaye ongoza kwa ufungaji hadi sasa.

Wachezaji wanaotoka ligi hiyo wamepachika wavuni magoli 11 na wengine kuzipa ushindi timu zao huku wengine wakitoa sare.

Cristiano Ronaldo (Real Madrid)

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, amefunga magoli 3 katika sare ya 3-3 dhidi ya Hispania mechi ya kwanza kabisa katika kundi lao lenye timu ya Iran na Morocco.

Nacho (Real Madird)

Katika mchezo huo Hispania dhidi ya Ureno naye amefunga goli bora kabisa, hadi sasa huenda ndio goli bora katika magoli yote yaliyofungwa.

Diego Costa (Atletico Madrid)

Naye alifunga magoli 2 katika sare ya 3-3 dhidi ya Ureno, Costa ni raia wa Brazil aliyebadili gia angani na kuchagua Hispania baada ya kuona nabii hakubaliki nyumbani.

Antoine Greizmann (Atletico Madrid)

Naye alifunga goli moja kwa mkwaju wa penati ambapo timu yake ya taifa ya Ufaransa ikichomoza na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Austria.

Luka Modric (Real Madrid)

Alifunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 71 ikishuhudiwa Croatia wakiilaza Nigeria mabao 2-0, mchezo ulitegemewa huenda Nigeria wangepindua meza kibabe.

José María Giménez (Atletico Madrid)

Beki wa kati wa Atletico Madrid naye alifunga goli pekee la ushindi dhidi ya Misri dakika za mwisho kabisa za mchezo huo ameipatia ushindi timu yake ya Uruguay.

Denis Cheryshev (Villarreal)

Mchezaji wa timu ya taifa ya Urusi na mfungaji wa goli la pili kombe la dunia mwaka 2018 dakika ya 43, ikumbukwe wa kwanza ni Yuri Gazazinskiy yeye amefunga dkika ya 12 ya mchezo.

Wakati England ikiwa na wafungaji watatu, Aguero, Pogba na Jidinak, mechi bado zinaendelea leo hii saa tisa Costa Rica dhidi ya Serbia.

Wachezaji wa Real Madrid pekee wametengeneza magoli 5 huku Atletico ikitengeneza 4.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.