Magufuli: Wachezaji Stars msikate tamaa Afcon

Magufuli: Wachezaji Stars msikate tamaa Afcon

25 June 2019 Tuesday 14:21
Magufuli: Wachezaji Stars msikate tamaa Afcon


Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
RAIS John Magufuli amewata wachezaji na viongozi wa Stars kutovunjika moyo kutokana na matokeo ya mchezo wa Senegal na amewataka kuongeza juhudi na kujituma zaidi katika mashindano ya Afcon 2019 yanayoendelea nchini Misri ili kuweza kupata matokeo mazuri zaidi.

Pia amemruhusu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenda nchini Misri kushuhudia mashindano hayo na awafikishie salamu zake kuwa wasikate tamaa.

Amesema hayo leo Juni 25, 2019 Kigamboni jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa ghala kuu na mitambo ya gesi ya kampuni ya taifa Gas Tanzania Ltd(LPG) ambapo alikuwa mgeni rasmi.

''Japo mmefungwa lakini tumewaona jinsi mlivyojituma, msivunjike moyo na matokeo ya mchezo, msikate tamaa kwani tumeowana mlivyocheza kwa kujituma, hivyo naamini  mtaweza kupata matokeo mazuri zaidi mkiwa na moyo huo huo wa utaifa, juhudi na kujituma,'' amesema rais na kuongeza 

"Licha ya Stars kufungwa 2-0 na Senegal ambayo ni timu  bora na namba moja Afrika na iliyosheeni wachezaji wa kimataifa, mmeonyesha mwanzo mzuri."

Amesema Stars inatakiwa kuombewa na kwamba ushindi  ni wa Watanzania wote na ikifungwa tumefungwa wote

Juni 27, 2019 Stars inatarajia kucheza mechi ya pili na timu ya Taifa ya Kenya na Julai 1, 2019 itamalizia  mechi na Algeria.

Updated: 26.06.2019 09:23
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.