Majaliwa, JK, Mabeyo kunogesha harambee Yanga

Majaliwa, JK, Mabeyo kunogesha harambee Yanga

14 June 2019 Friday 10:16
Majaliwa, JK, Mabeyo kunogesha harambee Yanga

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika hafla ya harambee ya kuchangia klabu ya Yanga Africans

Pia rais mstaafu Jakaya Kikwete, mkuu wa majeshi, Venas Mabeyo  ni miongoni mwa wageni waalikwa watakaokuwepo katika hafla hiyo inayotarajiwa kufanyika Juni 15, 2019 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Harambee hiyo imelenga kukusanya fedha zitakazosaidia shughuli za kiutendaji za klabu hiyo ikiwemo usajili wa wachezaji, imepanga kukusanya kiasi cha takriban bilioni 1.2

Kamati ya kufanikisha harambee  hiyo imesema umewashirikisha viongozi  hao wa kitaifa  kwa kuwa  ni wadau wa maendeleo ya soka na wapo mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo nchini. 

Pia wamezialika kampuni, mashirika, wafanyabiashara maarufu nchini  na wanachama ambao watakuwa tayari kuchangia.

Tayari baadhi ya matawi ya klabu ya Yanga  yameshatoa michango yao. Huku wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wakinunua tiketi.

Hamasa ya utoaji ilichagizwa zaidi na kocha wa  sasa wa timu hiyo, Mwinyi Zahera

Updated: 14.06.2019 14:39
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.