Majibu ya Simba juu ya kocha Masoud Djuma haya hapa

Majibu ya Simba juu ya kocha Masoud Djuma haya hapa

18 September 2018 Tuesday 06:45
Majibu ya Simba juu ya kocha Masoud Djuma haya hapa

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema leo itajulikana kama Kocha wake Msaidizi, Masoud Djuma kama atasafiri na kikosi kuelekea kanda ya ziwa au la.

Manara ameibuka na kufunguka baada ya kusambaa kwa taarifa mitandaoni kuwa Kocha huyo ataendelea kutoambata na kikosi cha timu hiyo katika safari za mikoani.

Ofisa huyo amesema mara baada ya kikosi kuondoka na ndege mapema leo itajulikana kama Djuma atakuwa katika msafara wa safari hiyo au la kwa maana bado timu haijaondoka.

Djuma alisalia Dar es Salaam huku ikielezwa alikuwa akiwanoa wachezaji waliokuwa wamebakia jijini humo kwa ajili ya mechi zingine za ligi.

Simba utaelekea Mwanza ambapo itakuwa na kibarua dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Septemba 20 na baadaye dhidi ya Mwadui FC, Septemba 22 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Shinyanga.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.