banner68
banner58

Majibu ya ukimya wa Yusuph Manji haya hapa

Majibu ya ukimya wa Yusuph Manji haya hapa

13 June 2018 Wednesday 11:25
Majibu ya ukimya wa Yusuph Manji haya hapa

Na Amini Nyaungo

Wakati Yanga wakisubiri kwa hamu kubwa jibu la aliyekuwa mwenyekiti wao Yusuphu Manji ili wajue waanzie wapi, kumeibuka maswali mengi sana kwanini hadi sasa amekuwa kimya huku kukiwa hakuna maelezo ya kutosha hasa baada ya wanachamawa klabu hiyo ya mitaa ya Twiga na Jangwani kukataa kujiuzulu kwake.

Azania Post imejitahidi kuwatafuta baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuweza kujua ukimya wake unasababishwa na nini na kama kuna hofu yoyote juu ya ukimya huo kwa klabu yao, lakini pia makundi mbalimbali ya facebook nayo yamegubikwa na mijadala juu ya ukimya huo, majibu yao yamekuwa kama hivi.

Haikosi Masawili huyu anaishabikia Yanga akiwa na kadi ya uanachama na alikuwepo katika mkutano mkuu siku ya Jumapili amesema, sio rahisi kutafsiri mambo mawili yanaweza kutokea.

“Nadhani anaweza akawa na maana kubwa kuwa kimya kwake, huenda amekataa kurejea lakini anataka kuisadia klabu kimya kimya, pia anaweza kukaa kimya kujikusanya ili aje na nguvu nyingine,” aliandika.

Mohamed Chungua naye amesisitiza kuwa Manji ni mtu wa Yanga wala ukimya wake sio tatizo sana, kinachotakiwa umoja ambao wameutengeneza siku ya mkutano uzidi kuendelea.

“Nafikiri Manji hawezi kuchomoa hata kidogo, anapenda sana Yanga, anachofanya kina maana kubwa sana, sasa kama angeongea mapema nyie waandishi mngepata wapi habari za Yanga, naamini ataibuka na kuja na njia nyingine hata akikataa katika Nyanja ya uongozi, atakuja na aina nyingine,” amesema.

Tunu Ally, naye amesema tatizo kubwa la Yanga pesa kama atatoa pesa wakati tunasubiri uwekezaji sio tatizo nadhani salamu ushaanza kuziona, kuna watu wameanza kusajiliwa mfano tunasikia mchezaji wa Gor Mahia Medy Kagere unadhani pesa zimetoka wapi. Ni Manji huyo hivyo hajaacha wala hakatai,” amesema.

Moja la kundi la Facebook Yanga community wamejadili kila mmoja anasema yake, maoni mengi yakiwa anarudi au anafanya kimyakimya hadi kuelekea uwekezaji.

Kutokana na kukaa kimya kwa Yusuphu Manji kwa hali ya kawaida kunaweza kuleta tafsiri nyingine nyingi ambazo wanachama wanaweza wakajiuliza, mosi amekataa, pili anajiandaa na mkakati tatu ameamua kuisaidia Yanga kimya kimya hadi hapo mabadiliko yatakapofanyika.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Alfred Faustine 2018-06-29 20:12:06

Hamna chakimyakimya wala nini BOSS KAGOMA Tuangalie mbele mda unakwenda tusibweteke ,kama vipi tukope hata sacos..

Avatar
Paschal wa Tabora itema 2018-07-10 11:23:34

Washabiki ndo huwa wanaumia said kama manji hataki aachie ngazi vinginevyo tutasingizia wachawi

Avatar
Ismail matimba wa chunyu -ruangwa 2018-07-12 13:36:23

Manji arud jangwani ili na sisi wanajangwani tulale usingizi kama zamani