Makonda Mgeni Rasmi Simba na Yanga

Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa

Makonda Mgeni Rasmi Simba na Yanga

Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa

27 April 2018 Friday 19:33
Makonda Mgeni Rasmi Simba na Yanga

Na Habakuki Urio

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda ndiye atakuwa mgeni rasmi wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga utakaochezwa Jumapili Aprili 29,2018 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Habari ya Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Cliford Ndimbo amesema kuwa Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni.

Ndimbo aliongeza kuwa tayari tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000,VIP B na C 20,000 na Mzunguko(Jukwaa la rangi ya Chungwa,Kijani na Bluu) 7,000.

“Tiketi zinapatikana kupitia Selcom” aliongeza.

Katika mchezo huo Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.