Makonda:Inaniuma wachezaji Stars kusemwa vibaya 

Makonda:Inaniuma wachezaji Stars kusemwa vibaya 

25 June 2019 Tuesday 11:50
Makonda:Inaniuma wachezaji Stars kusemwa vibaya 

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema anaumizwa na watanzania wakiwamo viongozi mbalimbali  kuwalaumu na kuwazungumzia vibaya wachezaji wa timu ya soka ya  taifa, (Taifa Stars).

Hatua hiyo ni kufuatia Stars kufungwa 2-0 na Senegal katika mashindo ya Afcon 2019 nchini Misri.

Ameeleza hayo leo Juni 25, 2019 Kigamboni jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa ghala kuu na mitambo ya gesi ya kampuni ya taifa Gas Tanzania Ltd.  Mgeni rasmi alikuwa ni rais John Magufuli.

"Inaniuma kuona watu wanawalaumu na kuwashutumu wachezaji wa Stars, hivi jiulize wewe umeifanyia nini timu ya taifa. Mheshimwa rais Magufuli kama itawezekana naomba utoe neno la faraja kwa wachezaji na timu ya taifa kwa ujumla,'' amesema Makonda ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati maalumu ya kusaidia taifa Stars.

Kauli ya makonda inakuja ikiwa ni siku  chache baada ya baadhi wabunge waliokuwepo nchini Misri kutoa shutuma kwa kocha Emanuel Amunike na wachezaji wa timu hiyo.

Miongoni mwa waliotoa maoni yao ni Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyesema  miongoni mwa sababu iliyochangia timu ya Taifa kupoteza mchezo ni lishe duni ya wachezaji wetu

Pia Ndugai alisema viongozi wengi wa soka na michezo mingine nchini siyo watu sahihi wa kuongoza.

Mbunge wa  jimbo la Chemba mkoani Dodoma, Juma Nkamia alimlaumu kocha Amunike kuwa hakustahili kuwa mkufunzi wa timu hiyo.

"Kocha Amunike bado hajafikia uwezo wa kufundisha timu ya taifa, hata  nilipokuwa Misri afisa mmoja wa michezo wa Nigeria alinidokeza kama mngeniuliza, nisingependekeza  Amunike kuwa kocha wa Stars,'' amesema

Juni 27, 2019 Stars inatarajia kukutana na timu ya taifa ya Kenya (Harambee) ikiwa ni mchezo wa pili kundi C. Siku hiyo hiyo Senegal na Algeria nao watakutana.
Harembee nayo ilifungwa goli 2-0 na Algeria.

Updated: 25.06.2019 14:31
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.