Malinzi wenzake waendelea kusota rumande

"Kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini shahidi aliekuwa ameandaliwa yuko kwenye mafunzo Geita"

Malinzi wenzake waendelea kusota rumande

"Kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini shahidi aliekuwa ameandaliwa yuko kwenye mafunzo Geita"

20 May 2019 Monday 14:54
Malinzi wenzake waendelea kusota rumande

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
KESI inayomkabili, aliyekuwa rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake  wanne imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na shahidi kuwa mafunzoni Mkoani Geita.


Wakili kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) Pendo Temu amedai leo Mei 20,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde kuwa kesi hiyo imekuja kwaajili ya kusikilizwa  lakini shahidi aliekuwa ameandaliwa yuko kwenye mafunzo Geita.


"Kesi imekuja kwaajili ya kuendelea na usikilizwaji shahidi tuliyekuwa tumemwandaa yuko kwenye mafunzo mkoani Geita tunaomba tarehe nyingine kwaajili ya kuendelea na usikilizwaji"amedai Wakili Temu.


Baada ya maelezo hayo Hakimu Kasonde aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 3 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji na kuutaka upande wa mashtaka kuleta mashahidi waliobaki.
Tayari mashahidi 13 wa upande wa Mashtaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo.


Mbali na Malinzi wengine ni meneja wa  Ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao Kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka 30 katika   kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335.


Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji wa fedha kuwa miongoni mwa mashtaka  ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku wenzao Zayumba na Frola wapo nje kwa dhamana.
 

Updated: 20.05.2019 20:02
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.