Mambo yakufahamu ufunguzi wa Kombe la Dunia Urusi dhidi ya Saudi Arabia

Mambo muhimu kuyajua kabla ya mchezo

Mambo yakufahamu ufunguzi wa Kombe la Dunia Urusi dhidi ya Saudi Arabia

Mambo muhimu kuyajua kabla ya mchezo

14 June 2018 Thursday 14:47
Mambo yakufahamu ufunguzi wa Kombe la Dunia Urusi dhidi ya Saudi Arabia

Na Amini Nyaungo

Hatimaye kombe la Dunia lishafika baada ya kusubiria kwa miaka minne wanamichezo na watu wengine duniani watakaa sehemu moja kuangalia michuano hiyo.

Mchezo huo utachezwa saa 12 joni kwa saa za Afrika Mashariki na kati, itaanza sherehe mablimbali ikifuatiwa na mchezo wenyewe.

Watazania wengi wanapenda mchezo wa soka, wanapenda kuangalia sehemu moja inayofahamika kama `Vibanda umiza`, wanaamini wakikaa hapo watafurahi hasa kwa kuzomeana kutokana na uchaguzi wa timu zao.

Bingwa mara nyingi wa michuano hiyo ni Brazil ambaye amechukua mara 5 akifuatiwa kwa karibu na Ujerumani na Italia wote wamechukua mara nne.

Mambo muhimu kuyajua kabla ya mchezo ni haya yafuatayo;

Nestor Pitana

Ni mwamuzi mzoefu kutoka Argentina ndiye atakayesimama kufungua mchezo wa leo kati ya Urusi dhidi ya Saudi Arabia.

Néstor Fabián Pitana ameorodheshwa na FIFA mwaka 2010 ana miaka 42 na hili ndio litakuwa kombe lake la mwisho la Dunia maana ikifika miaka 45 huwa chama cha soka Duniani FIFA huwavua Beji yao.

Rusia dhidi ya Saudi Arabia

Mchezo wao wa kwanza ilikuwa mwaka 1993, Saudi Arabia ilishinda 4-2 katika uwanja wake wa nyumbani, lakini hii ilikuwa mchezo wa kirafiki.

Tangu Urusi ilivyogawanyika haijawahi kufika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo mara tatu walizoshiriki 1994, 2002 na 2014.

Saudi Arabia mara zote walizoingia kushiriki michuano hii imeshika nafasi ya mwisho katika makundi yao.

Stanislav Cherchesov (Urusi) dhidi ya Juan Antonio Pizzi (Saudi Arabia)

Hawa ndio makocha watakao simama mchezo wa leo ambapo mataifa yao wamewachagua kuongoza.

Luzhniki

Huu ndio uwanja utakaofungua kombe la dunia siku hii ya leo ambapo una historia kubwa kama tulivyowahi kuziorodhesha katika Makala zetu.

Kundi hili linaundwa na Misri, Urusi, Saudi Arabia na Uruguay, leo ni mchezo mmoja tu nyingine itachezwa siku ya kesho. Timu mbili za juu ndizo zitakazo nufaika kuingia hatua ya mtoano ambayo huwa inafahamika kama 16 bora.

Wachambuzi wengi wanazipa nafasi timu tano ikiwa Ujerumani, Brazil, Ufaransa, Argentina na Ubelgiji.

Dola bilioni 18 imetumika kuweza kuandaa michuano hiyo kuanziautengenezaji wa viwanja na mambo mengine ya hoteli, ni gharama kubwa sana kuwahi kutokea katika kombe hili.

Azania Post

Updated: 14.06.2018 14:55
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.