Man United yakataa kitita usajili wa Lukaku

Man United yakataa kitita usajili wa Lukaku

20 July 2019 Saturday 21:50
Man United yakataa kitita usajili wa Lukaku

Manchester United imekataa dau la pauni milioni 53.9 kutoka kwa Inter Milan walizotaka kuzitoa kumnunu mshambuliaji wake, Mbelgiji Romelu Lukaku.

Miaka miwili iliyopita Man United ilimnunua mshambuliaji huyo  mwenye umri wa miaka 26 kwa paundu milioni 75 kutoka Everton

Mkufunzi wa Inter Milan, Antonio Conte amemfanya Lukaku kama chaguo lake la kwanza katika usajili wake

"Mnajua ninmpenda mchezaji huyu ," alisema Conte  na kuongeza "Nilipokuwa kocha wa Chelsea, nilijaribu kumleta Chelsea.

"Ninampenda mchezaji huyu, na ninamchukulia kama mchezaji muhimu kwetu ili kuweza kupata mafanikio, lakini wakati huo huo kuna soko la uhamisho.

"Tutaona kitakachotokea -lakini kwa sasa Lukaku ni mchezaji wa United ."

Hatua ya Inter Milan ya kumtaka Lukaku inamuonyesha njia mshambuliaji wa sasa wa timu hiyo Mauro Icardi, ambaye hajasafiri katika safari  barani Asia ya maandalizi ya  msimu huu huku kukiwa na ripoti kuwa ataondoka.

Alipoulizwa kuhusu mshambuliaji wa Argentina , Conte alijibu : "klabu iko wazi kwamba Icardi yuko nje ya mradi wa Inter Milan. Hii ndio hali halisi ."

Aliposhinikizwa kuhusu hali ya baadae ya Lukaku, Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alisema kuwa "sina taarifa mpya".

Mbelgiji huyo alikosa ,mechi zote za Manchester United ilipocheza nchini Australia kutokana na majera "Hayuko fiti. Hatakuwepo,"alisema Solskjaer.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.