Man United yashindwa kuongoza Ligi EPL

Man United yashindwa kuongoza Ligi EPL

20 August 2019 Tuesday 04:46
Man United yashindwa kuongoza Ligi EPL

TIMU ya Man United imeshindwa kupata nafasi ya kuongoza ligi baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Wolves katika mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza(EPL) uliochezwa usiku wa kuamkia leo Agosti 20, 2019.

Man United ilikuwa ya kwanza kupata goli kunako dakika ya 27 kupitia kwa mshambualiaji Mfaransa Anthony Martial lakini Wolves wakachomoa kunako dakika ya 55 kupitia kwa Ruben Neves na kuifanya Man United kushindwa kupata nafasi ya kuongoza Ligi. Ushindi wa aina yoyote ungeiwezesha Man United kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli. Livepool sasa  wanaongoza ikiwa na ponti 6 michezo miwili

Huo ni mwendelezo  wa Wolves, simu uliopita wa mwaka 2018/2019 Man United ilipokea vipigo viwili mfululizo kutoka kwa Wolves katika mchezo wa Ligi Kuu na Kombe la FA.

Mara ya mwisho kwa Man United kumfunga Wolves ilikuwa Machi 18, 2012 chini ya kocha Sir Alex Furgason katika mchezo wa Ligi Kuu England ambapo Man United walipata ushindi wa magoli 5-0.

Man United na Wolves waamekutana mara 102, Wolves akishinda mara 36 na Man United mara 48 huku sare zikiwa 18. Man United walikuwa ugenini

Updated: 20.08.2019 05:05
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.