Mandawa aigomea klabu yake

Mandawa aigomea klabu yake

12 June 2019 Wednesday 00:00
Mandawa aigomea klabu yake

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Rashid Mandawa (25) ameigomea klabu yake ya BDF XI kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia maafande hao wa Botswana.


Mandawa ameibuka na kuongelea hilo kwa njia ya simu, akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stats' nchini Misri ambako wanajiandaa na fainali za mataifa ya Afrika 'AFCON'.


Mandawa alisema taarifa zilizozaa kuwa ametemwa na BDF XI ni uzushi mtupu kwa sababu klabu hiyo ilimtaka aongeze mkataba wa kuendelea kuichezea.


"Msimu ulivyoisha nilikaa na kuongea na kocha kuwa nahitaji kupiga hatua zaidi kwa kwenda sehemu nyingine ambayo naweza kukumbana na changamoto mpya za soka.


"Alihitaji kuendelea kufanya kazi na mimi lakini nashukuru mungu kwa sababu alinielewa hivyo ameniondoa kwenye mipango yake ya msimu ujao sijatemwa kwakweli," alisema Mandawa.


Mandawa alisema anajivunia mengi aliyojifunza akiwa Botswana na katu hawezi kuisahau BDF XI kwa heshima kubwa na imani waliyokuwa nayo juu yake.


"Nilikuja kufanya majaribio huku tena haikuwa BDF XI, ilikuwa Township Rollers nilipofeli, wao waliamua kunisajili nilistuka kumbe walikuwa wakitambua uwezo wangu, hawakutaka nifanye majaribio.


"Nimekuwa na maisha mazuri BDF XI lakini naamini ni wakati sahihi kwangu kufungua ukurasa mwingine kwenye soka langu, nashukuru kwa benchi zima la ufundi, wachezaji na mashabiki kwa upendo wenu," alisema.


Ndani ya msimu huo, Mandawa atakumbukwa kwa mabao yake matatu 'hat trick' aliyofunga mbele ya Township Rollers ambao walishindwa kumsajili baada ya kufanya majaribio.
Mandawa anadai kuwa anaofa kibao ambazo amepata na miongozi mwa ofa hizo kuna timu ambayo inashiriki Ligi Kuu Afrika Kusini 'PSL'.


"Baada ya Afcon naweza kusema wapi nitaenda ila sio tena kurejea nyumbani, sina hayo mawazo kwa sasa," alisema Mandawa ambaye aliwahi kuichezea Mtibwa Sugar

Updated: 12.06.2019 14:22
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.