Manula, Nyoni, Kapombe wasaini tena Simba

Manula, Nyoni, Kapombe wasaini tena Simba

12 June 2019 Wednesday 13:57
Manula, Nyoni, Kapombe wasaini tena Simba


Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
KIPA Aishi Manula, mabeki Erasto Nyoni na Shomari Kapombe wamesaini mikataba mipya kuendelea kuitumikia timu ya Simba.

Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu ya Simba zimebainisha kuongezwa mikataba wachezaji hao, licha ya kuhofia kuweka wazi ni ya muda gani.

"Makubalino ya ndani ni kwamba habari zote zitatolewa 'official' hivyo kwa kifupi wachezaji hao wamekwishasaini Simba pamoja na Bocco (Mei 17), lakini mikataba ya muda gani, taarifa rasmi zitatolewa kulingana na makubaliano," kimesema chanzo cha kuaminika ndani ya klabu hiyo.


Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori alipoulizwa kuhusu kuongezwa mikataba wachezaji hao amesema zoezi la kuwaongezea mikataba wachezaji wao linaendelea kila siku tangu juzi.


"Hiki ni kipindi cha kuwaongeza mikataba wachezaji ambao tunabaki nao, kila kitu kitakuwa wazi na Leo saa 7 Mchana (Jana) tutamuongeza mchezaji mwingine mkataba, zoezi litafanyika kila siku hadi idadi tunayohitaji itakapotimia," alisema," Magori.


Amesema baada ya kuwaongeza mikataba, itatangaza wachezaji wanaoachwa, kisha wapya watakaosajiliwa kipindi hiki cha dirisha kubwa.

Updated: 13.06.2019 07:10
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.