banner68
banner58

Mashabiki Simba wamzomea Fei Toto Uwanja wa Taifa

Mashabiki Simba wamzomea Fei Toto Uwanja wa Taifa

13 July 2018 Friday 20:16
Mashabiki Simba wamzomea Fei Toto Uwanja wa Taifa

Feisal Salum Ab­dallah ‘Fei Toto’ amekutana na wakati mgumu wakati mashabiki wa Simba walipomzomea.

Mashabiki wa Simba walimzomea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati akiitumikia timu yake ya JKU ya Zanzibar dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Fei Toto alikuwa akiitumikia JKU katika mechi ya Kombe la Kagame kuwania kupata mshindi wa tatu.

Lakini mashabiki wa Simba walikuwa wakimzomea kwa nguvu kila aliposhika mpira.

Mashabiki hao walikuwa uwanjani wakati wakisubiri mechi ya fainali, Simba ikisubiri kuivaa Azam FC ambayo ndiyo kinara kwa maana ya bingwa mtetezi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.