Matukio saba ya kusisimua uwanja wa ufunguzi Kombe la Dunia Urusi

Vitu muhimu unavyotakiwa kujua kuhusu uwanja huo tangu kujengwa kwake

Matukio saba ya kusisimua uwanja wa ufunguzi Kombe la Dunia Urusi

Vitu muhimu unavyotakiwa kujua kuhusu uwanja huo tangu kujengwa kwake

02 June 2018 Saturday 14:22
Matukio saba ya kusisimua uwanja wa ufunguzi Kombe la Dunia Urusi

Na Amini Nyaungo

Zimesalia siku 12 kuelekea ufunguzi wa kombe la dunia katika uwanja wa Luzhniki, ambao ni moja ya viwanja vikongwe huko nchini Urusi.

Uwanja huo ulijengwa mwaka 1956, kwa lengo la kufanyia shughuli tofauti za kijamii. Hapa ndipo sherehe za ufunguzi wa michuano hii mikubwa Zaidi ya soka ulimwenguni itafanyika, na baadae mchezo wa kufungua pazia baina ya wenyeji Urusi dhidi ya Saudia Arabia ukipigwa.

Kwa muda mrefu uwanja huo umekuwa ukitumika kwa shughuli za kitamaduni nchi humo, pia ulitumika katika kutafuta vipaji kwa wachezaji chipukizi wa soka. Tukio kubwa ambalo limewahi kufanyika uwanjani hapo ni michezo ya Olimpiki yam waka 1980.

Vitu muhimu unavyotakiwa kujua kuhusu uwanja huo tangu kujengwa kwake;

Watumika kisiasa, wabadilishwa jina

Kabla ya uwanja huo kukarabatiwa vizuri mwaka 1956, ulikuwa unatumika kwa shughuli za kiserikali. Kuanzia mwaka 1950 hadi 1960, ulikuwa na uwezo wa kuingiza wanachama 100,000 wa chama cha Kikomunisti enzi za Umoja wa Kisoviet.

Mwaka 1992, uwanja huo ulibadilishwa jina kutoka Lenin hadi Luzhniki, kwa lengo la kuendana na jina la kitongoji cha Luzhniki, kilichopo katikati ya jiji la Moscow.

Wapunguzwa, waongezwa viti

Uwanja huo ulikuwa na uwezo wa kuingiza watu 100,000 baada ya marekebisho makubwa yaliyofanyika mwaka 1960, yaliufanya uwanja huo kuwa na uwezo wa kuingiza watu 78,000.

Baada ya nchi ya Urusi, kupata nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia, mwaka 2013 uwanja huo ulifanyiwa ukarabati mkubwa kwa kuongezwa viti 3,000 na kufikisha idadi ya viti 81,000.

Eneo kubwa latumika kuukarabati

Ukarabati uliofanyika mwaka 2013, ulichukua eneo kubwa sana.

Uwanja huo ambao upo katika Mji wa Moscow, ulitumia eneo la hekta 180 na kuishia kando ya mto Moskova, uliopita karibu na uwanja huo.

Pamoja na kuchukua eneo kubwa, uwanja huo ndio wenye uwezo wa kuingiza watazamaji wengi na pia ndani yake kuna viwanja vingi vya michezo mingine ambayo hutumika katika michuano ya Olimpiki.

Mgogoro wazuka mwaka 2017

Wakati uwanja huo umemalizika, baadhi ya viongozi wa serikali nchini humo walitaka utumike katika michezo ya Kombe la Mabara, ambalo lilifanyika nchini humo mwaka 2017.

Pamoja na shinikizo la Serikali, rais wa Shirikisho la Mpira wa Urusi, Vitaly Mutko, alikataa kabisa uwanja huo kutumika na aliamua kuteua viwanja vinne ambavyo vilitumika katika michuano hiyo ya Kombe la Mabara.

Viwanja hivyo ni Saint Petersburg, Moscow, Kazan na Sochi.

Manchester United, Chelsea wautumia

Fainali ya UEFA Champions League ya mwaka 2008 ilifanyika katika uwanja huo wa kihistoria nchini Urusi.

Manchester United ilifanikiwa kutwaa kombe hilo kwa ushindi wa mikwaju penalti 6-4.

Pia mwaka 1999, ilifanyika fainali ya Europa League, wakati ule inajuliakana kama EUFA Cup. Mchezo huo ulizikutanisha Parma na Marseille, na Parma alishinda kombe hilo kwa mabao 3-0.

Watu 66 wafariki uwanjani

Mwaka 1982, katika mchezo wa UEFA Cup kati ya Sparta Moscow dhidi ya HFC Haarlem, watu 66 walifariki katika uwanja huo na tukio hilo kuwa tukio baya zaidi lililowahi kutokea katika mchezo wa soka nchini Urusi.

Chanzo cha vifo cha watu hao kilitajwa kuwa ni mlundikano wa watu wengi katika eneo moja ulisababisha maafa hayo.

Mechi saba kuchezwa

Katika michezo ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Urusi, uwanja huo utatumika kwa michezo saba tu ikiwamo mchezo wa ufunguzi na fainali ya kombe hilo.

Michezo hiyo ni Urusi v Saudi Arabia, Ujerumani v Mexico, Ureno v Morocco, Denimark v Ufaransa, huku michezo mingine mitatu itapigwa baada ya hatua ya makundi kumalizika.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.