Mbenin wa Yanga asepa, atoa mazito juu ya soka la Tanzania

Asema soka la Tanzania haliwezi kuendelea iwapo...

Mbenin wa Yanga asepa, atoa mazito juu ya soka la Tanzania

Asema soka la Tanzania haliwezi kuendelea iwapo...

29 June 2018 Friday 18:33
Mbenin wa Yanga asepa, atoa mazito juu ya soka la Tanzania

Na Amini Nyaungo

Habari hii ya moto kabisa ambayo kupitia ukurasa wa Instagram wa mchezaji ambaye alitazamiwa kuziba pengo la Obrey Chirwa Mbenini Marcellin Koukpo ameonekana ameposti picha akiwa katika ndege huku akiweka ujumbe mzito.

Mchezaji huyo ameposti picha akiwa katika ndege ndege akisema kuwa mpira wa Tanzania hautoweza kuendelea kutokana na watu wa kati.

Kwa kutumia lugha ya Kiingereza, mshambuliaji huyo raia wa Benin alisema, “Bye Bye,” ikiwa ni kama anaaga.

Baada ya watu kutoa maonı yao akajıbu kuwa, “Tanzania football will drom due to the middlemen in the football industry,” akiwa anamaanishwa kwamba, soka la Tanzania siku zote litaendelea kwenda chini sababu ya madalali walioko katika mpira.

Kwa kauli hii inaonesha dhahiri kwamba mchezaji huyo amechemka Yanga na anarejea kwao.

Koukpo alikuja kufanya majaribio kwa ajili ya kujiunga na Yanga na ni wiki sasa alikuwa jijini Dar es Salaam alikokuwa anasubiriwa na kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera.

Kwa kauli yake hiyo ya watu wa kati wewe umeilewaje, haya kama kawaida toa maoni yako kupitia ukurasa wa Instagram, Twitter na Facebook utuambie umeelewaje.

Azania Post

Updated: 29.06.2018 18:44
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Abdul 2018-06-29 19:16:39

Walitaka wamdalalie kwenye usajili wake wabongo ndivyo tulivyo

Avatar
petro mwasindikila 2018-06-29 20:57:42

kamati ya usajili haijaturia haiwezi kutuambia kwamba tunasajiri kimyakimya mbona wachezaji wanaondoka

Avatar
Mussa kazimil 2018-06-30 00:02:29

Hakika liwe funzo kwa viongozi wetu kwani huyu jamaa siyo kashindwa kucheza lakini huenda namna timu zinavyoongozwa na hawa viongozi wetu. Wakae watumie kasolo ndogondogo kama hizi kutatua matatizo ya timu na siyo ulaji tuu!!!
Moira bongo ni kichwa cha mwenda wazimu(mwinyi)

Avatar
LAMECK DAUD 2018-07-06 10:52:54

Ni kwel kwan hata mm naungananae kwa soka la bongo kamwe haliwezi kuendelea kwa sababu tumeweka usiasa mpaka kwenye soka

Avatar
Mjele 2018-07-08 23:58:12

kashindwa tu? ila wabongo tuache fingisu kwa maisha ya soka

Avatar
Ismail matimba 2018-07-12 13:42:25

Yatupasa kufanya mabadiliko juu ya mapungufu hayo

Avatar
Abel Mwendesha 2018-07-29 23:51:59

huo ndio ukwel bila kubadilisha mwenendo soka letu halina pakwenda mbali watakomemea kuwaona kwenye mazoezitu