Mbivu, mbichi kesi ya Malinzi wenzake kujulikana Julai 23

Mbivu, mbichi kesi ya Malinzi wenzake kujulikana Julai 23

12 July 2019 Friday 15:45
Mbivu, mbichi kesi ya Malinzi wenzake kujulikana Julai 23

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

HATMA ya aliyekuwa rais wa shirikisho la soka nchini ((TFF), Jamal Malinzi na wenzake wanne kama wana kesi ya kujibu ama la itajulikana Julai 23, 2019.

Uamuzi huo umetolewa leo Julai 12, 2019   katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde baada ya Jamhuri kufunga ushahidi.

Akiiwakilisha Jamhuri Wakili wa Serikali kutoka Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amedai kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na wanania ya kufunga ushahidi.

“Mheshimiwa upande wa mashtaka tunaomba kufunga ushahidi kwa upande wetu,”alidai Swai na mahakama ilikubali. Upande huo ulikuwa na mashahidi 15 waliotoa ushahidi.

Mahakama imeamuru kuwa Julai 23, 2019  itatoa uamuzi wa kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama la  na endapo watakutwa na kesi ya kujibu watatakiwa kuanza kujitetea.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Meneja wa Ofisi TFF, Miriam Zayumba, Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola za Marekani 173,335.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wanaendelea kusota rumande kwa sababu wanakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Updated: 12.07.2019 15:55
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.