Mbwana Samatta kurudi Simba

Mbwana Samatta kurudi Simba

31 May 2019 Friday 10:58
Mbwana Samatta kurudi Simba

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MBWANA Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema atamalizia soka lake akiwa na timu ya soka ya Simba baada ya kustaafu kucheza soka la kimataifa.

Ametoa kauli hiyo jana Mei 30, 2019  alipokuwa katika tuzo za Mo Simba award na ameitaka Simba kufanya vizuri katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika.

"Simba kuchukua ubingwa nchini si hoja, sasa waongeze nguvu zaidi ili wapate mafanikio zaidi katika mashindano ya klabu bingwa Afrika,''amesema na kuongeza " Nitamalizia soka langu katika klabu ya Simba labda wanikatae wenyewe.

Samatta ambaye ni mshambuliaji wa CRG genk ya nchini Ubelgiji amewataka wachezaji nchini kujituma zaidi ili kufanikiwa wao na ili kiwango cha soka nchini kiongezeke.

Amesema tuzo za klabu za Mo Simba award zinaongeza ari na motisha.

Mchezaji huyo yupo nchini kwa ajili ya maandilizi ya timu ya taifa kushiriki michuano ya Afcon 2019 itakayochezwa nchini Misri mwezi Juni. 

Taifa Star ipo kundi C ikiwa na timu ya Senegal, Kenya na Algeria

Taifa Star inatarajiwa kuanza kambi Juni 1, 2019  na inatarajiwa kuondoka nchini Juni 7, 2019 ikiwa na wachezaji 27.

Kwa sasa kocha wa timu hiyo mnaigeria Emmanuel Amonike amewaita wachezaji 33 na watafanyiwa mchujo.

Updated: 01.06.2019 08:48
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.