banner68
banner58

Mbwana Samatta mambo yaelekea kuwa safi England

Mbwana Samatta mambo yaelekea kuwa safi England

11 October 2018 Thursday 06:28
Mbwana Samatta mambo yaelekea kuwa safi England

Imeelezwa kuwa klabu ya Everton ambayo inashiriki Ligi Kuu ya England, ina mpango wa kumsajili mshambuliaji Mbwana Samatta, ambaye anakipiga katika Klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji.

Timu hiyo inataka kumsajili mche­zaji huyo ili aweze kuziba pengo la Oumar Niasse ambaye anataka kuondoka katika klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Liverpool nchini Uingereza baada ya kushindwa kupata namba ya kudumu katika misimu ya hivi karibuni.

Samatta ambaye anaonekana msimu huu kuwa moto kutokana na kufanya vyema kwenye michuano tofauti, mpaka sasa katika michua­no ya Europa amefunga mabao sita huku akifunga mabao saba kwenye ligi.

Nyota huyo amekuwa kwenye kiwango bora kwa sasa na tayari msimu huu ana ‘hat trick’ mbili al­isajiliwa Genk akitokea Klabu ya TP Mazembe ya nchini DR Congo.

Everton kwa sasa inasaka msham­buliaji mbadala wa Oumar Niasse, na tayari kocha wa timu hiyo, Marco Silva, ameonekana kuvutiwa na kasi wa Samatta.

Hata hivyo, jana iliripotiwa na vyombo mbalimbali vya Ulaya kuwa mbali na Everton pia West Ham United, Burnley na Brighton wame­kuwa wakiwania saini ya nyota huyo kutokana na uwezo ambao ame­kuwa akionyesha kwa sasa.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.