banner68
banner58

Mbwana Samatta mbioni kutimkia La Liga

Kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza moja ya ligi kubwa tano duniani akifanikiwa

Mbwana Samatta mbioni kutimkia La Liga

Kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza moja ya ligi kubwa tano duniani akifanikiwa

27 July 2018 Friday 14:08
Mbwana Samatta mbioni kutimkia La Liga

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania na KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta yupo kwenye mazungumzo na Klabu ya Levante inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania ‘Laliga’ kukamilisha mpango wa kuhamia klabuni hapo.

Levante imetenga kitita cha Euro milioni 4 ili kumnasa Samatta, japo klabu yake anayoitumikia KRC Genk, imekataa ofa hiyo na kuhitaji Euro milioni 8.

Iwapo atafanikiwa kutimkia huko, basi atacheza Ligi moja na mwamba wa soka wa Dunia, Lionel Messi wa Barcelona.

Wakala wa Samatta amethibitisha kuwepo kwa mazungumzo baina ya klabu hizo mbili huku miamba ya Urusi klabu ya CSKA Moscow imekuwa ikihitaji huduma ya kijana huyo Mtanzania.

Samatta lipojiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea katika miamba ya soka ya Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
JOHN ELIAS 2018-07-27 21:47:07

kila lakheri watanzania tupo nyuma yako, god bless you brother

Avatar
Iddi Mbegu 2018-07-28 17:39:04

iyo ni furaha kubwa kwa watanzania wote kuona mtanzania anachezea ligikuu ya LALIGA ya SPAIN

Avatar
miraj mchemia 2018-08-01 20:21:20

safi sna mbwana samata

Avatar
mgindo mgindo 2018-08-02 08:56:20

nenda ukajaribu bahati yako

Avatar
Benjamin joseph 2018-08-02 20:13:59

kila laheri mbwana samatta endapo utafanikiwa kucheza ligi kubwa kama La liga na itakuwa furaha kwetu watanzania kuona samatta akicheza spain na kutakuwa na hamasa kwa wachezaji wengine wa kitanzania kuona kitu kama hicho.mungu amubariki samatta huko aendako

Avatar
Alanus kalunga 2018-08-04 07:48:49

Mungu akusaidie sana samatta katuwakilishe watanzania

Avatar
tekn barack 2018-08-04 13:57:27

inshala brother

Avatar
Maseke nyaheri 2018-08-08 21:14:20

Hongera dogo langu tunakuombea kwa God uiwakilishe tanzania yetu.org.