banner68
banner58

Mchezaji huyu Yanga yuko 'fiti' kuikabili Simba

Mchezaji huyu Yanga yuko 'fiti' kuikabili Simba

25 September 2018 Tuesday 12:45
Mchezaji huyu Yanga yuko 'fiti' kuikabili Simba

Baada ya baadhi ya taarifa kuibuka zikieleza kuwa kiungo fundi na mjanja wa klabu ya Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' kuwa atakosekana kwenye mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba, uongozi Yanga umethibitisha atakuwepo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, ameeleza kuwa Toto atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachocheza na Simba Septemba 30, 2018.

Toto amekuwa pia mmoja wa wachezaji walioelekea mjini Morogoro jana kwa ajili ya kambi maalum kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba.

Yanga imeamua kuliacha jiji ili kuwapa utulivu wa aina yake wachezaji wake pia kuwaweka fiti kisaikolojia kwa ajili ya ajili ya kuhakikisha wanapigania alama tatu dhidi ya Simba.

Kikosi hicho kitarejea Dar es Salaam majira ya jioni Septemba 29 tayari kwa ajili ya kucheza na Simba Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
rweyemamukatunzi46@gmail.com 2018-09-25 16:00:52

Hata kama hatacheza. Wapo vijana wengi namba za kati

Avatar
Joseph Douglas simba 2018-09-26 10:55:25

Safi sana tunaiombea Tim yetu ipate ushindi hiyo tarehe 30.09.2018